Tuesday 17 May 2016

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE 11 KUNUSURIKA BAADA YA KULA WALI MAHARAGE MKOANI GEITA


Mtu mmoja amefariki dunia na wengine  kumi na mmoja kunusurika kifo baada ya kumaliza kula chakula cha usiku.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jumatatu katika kata ya Nyarugusu mkoani Geita ambapo inadaiwa kuwa watu hao baada ya chakula cha usiku ambacho ni wali maharage walijikuta wakianza kuumwa na tumbo  hali ambayo ilisababisha wote kwa pamoja kuanza kuharisha.

Akizungumzia tukio hilo baba wa familia hiyo bw, Gulamali Fungameza amesema kuwa baada ya hali hiyo kutokea waliamua kwenda katika hospitali teule ya mkoa wa Geita ili kupatiwa matibabu lakini mmoja kati ya watu hao aliyefahamika kwa jina la Rejiko Shija alifariki dunia kabla ya kuanza kupatiwa matibabu.

Hata hivyo pia ,mmoja kati ya watu waliosalimika ,aliyejitambulisha kwa jina la Joyce  Johachim,amesema kuwa tatizo hilo limetokana na mgonjwa ambae alikuja nyumbani hapo  akitokea mjini Geita ambapo alifika  akiwa na ugonjwa wa kuharisha na kutapika hali ambayo ilisababisha familia nzima kujikuta wakiingia katika ugonjwa huo.

Aidha mganga mfawidhi wa hospitali teule ya rufaa mkoani hapa dr. Adam Sijaona,amekiri kupokea wagonjwa hao na kwamba amedai hadi kufikia hivi sasa chanzo cha tatizo hilo bado hakijafahamika.
cue…………..…………..sijaona

No comments:

Post a Comment