Monday 30 May 2016

WABUNGE 7 WA UPINZANI WASIMAMISHWA KUHUDHURIA BUNGENI

Akisoma maamuzi hayo ya Bunge Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, George Mkuchika amesema Januari 27.01.2016 wabunge hao walikiuka sheria na taratibu za kuongoza bunge kwa walishinikiza kiti cha spika kijadili hoja ambayo ilikwisha tolewa uamuzi na kiti hicho.

Wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao hivyo ni Zitto Kabwe, John Heche, Halima Mdee, Tundu Lissu, Godbless Lema, Pauline Gekul na Esther Bulaya.

Azimio la adhabu kwa wabunge hao limetolewa na Bunge chini ya Kifungu cha 30A (1) cha sheria ya Haki Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na kanuni ya 74 (4) na (6).

Kufuatia uchunguzi huo Bunge kupitia kamati hiyo limeazimia kuwa Ester Bulaya naTundu Lisu wasihudhurie vikao vyote vya mkutano wa tatu wa Bunge la Kumi na Moja vilivyobaki kuanzia tarehe 30 Mei , 2016 pamoja na vikao vyote vya Mkutano wa Nne Spika wa Bunge la Kumi na Moja kwa kuwa walipatikana na makosa ya ukiukwaji wa Kanuni na kuonyesha dharau kubwa kwa mamlaka ya Bunge.

Aidha, Bunge limeazimia kuwa Mhe. Pauline Gekul, Mhe.Godbless Lema, Mhe.Zitto Kabwe na Mhe Halima Mdee wasihudhurie vikao vyote vya mkutano wa tatu wa Bunge kuanzia tarehe 30 Mei 2016.
Adhabu hizo Bunge limeazimia Mhe.John Heche asihudhurie vikao kumi mfululizo vya Mkutano wa Tatu wa Bunge hilo kuanzia Mei, 30, 2016 kwa kuwa alipatikana na kosa moja.


No comments:

Post a Comment