Tuesday 10 May 2016

WANANCHI KATA YA NYANGOKO WAISHUKURU HALMASHAURI YA MJI WA GEITA KWA KUJENGA KISIMA CHA MAJI

Wananchi  wa mtaa wa Nyakato  kata ya Nyangoko wilayani na mkoani Geita,wameishukuru halamshauri  ya mji na diwani wa kata hiyo kutokana na jitihada ambazo  wamezifanya za kuhakikisha kuwa kisima cha maji kinapatikana katika mtaa  huo.

Wakizungumza na Storm habari,baadhi ya wananchi wa mtaa huo,wamesema kuwa  ni kwa muda mrefu wamekuwa wakikutana na adha kubwa kutokana na ukosefu wa maji katika mtaa huo lakini kwa sasa kutokana na  kufunguliwa kwa kisima cha maji kitawasaidia kutumia kwa shughuli za nyumbani.

Mwenyekiti wa mtaa huo,Charles  Kulola amesema kuwa mradi huo utawanufaisha wananchi zaidi ya elfu 2,600,na mwalimu wa shule ya msingi  Nyakato Peter Mpandoji yeye  ameelezea namna ambavyo wanafunzi walikuwa wakikumbana na adha kutokana na kuwepo kwa uhaba  wa maji hali ambayo ilikuwa ikisababisha  wanafunzi wengi kuwa watoro.


Aidha kwa upande  wake diwani wa kata ya Nyangoko,Elias  Ngole amesema kuwa mradi huo ni moja kati  ya mwendelezo wa  halmashauri wa kuhakikisha kuwa wanatumia mapato ya ndani na kiasi cha sh,milioni thelathini     zimetumika kutengeneza mradi huo.

No comments:

Post a Comment