Thursday 12 May 2016

SEKTA YA WAUGUZI KUENDELEA KUKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI

Ikiwa  leo nchi  inaadhimisha siku ya wauguzi  bado sekta hiyo imeendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na maeneo ya  kuishi kutokuwa na usalama,,sare za kazi zao kuendelea  kujishonea wenyewe pamoja na kuwepo kwa maslahi duni  katika sekta hiyo.


Akizungumzia changamoto hizo katika siku ya wauguzi ambayo kitaifa imefanyikia mkoani Geita Raisi wa chama cha wauguzi na wakunga nchini,Paul Magesa,amesema kuwa pamoja na jitihada za kutoa huduma kwa wananchi  changamoto nyingi zimeendelea kuwakabili  ikiwemo swala la wauguzi kupigwa  na pia swala la viongozi wa kisiasa kuendelea kuingilia sekta hiyo.

Aidha kwa upande wake, waziri wa nchi ofisi ya rais, tawala za mikoa na serikali za mitaa mh George Simbachawene amewaagiza wakuu wa mikoa wote nchini kuhakikisha kwamba wanazisimamia halmshauri zote na kuhakikisha kuwa wanawalipa fedha na kununua sare kwa ajili ya watumishi hao zitokanazo na mapato ya ndani.

Kwa upande wake ,makamu wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambae alikuwa ni mgeni rasimi katika maadhimisho hayo mh Samia Suluhu Hassani  ,amewataka viongozi wa serikali na wa kisiasa kufuata taratibu zote za kiutumishi katika kubaini makosa kwa wauguzi wanaotuhumiwa kabla ya kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kusikiliza pande zote mbili.


Siku kuu ya wauguzi uadhimishwa kila ifikapo mei 12 ya kila mwaka,lengo ikiwa ni kukumbuka misingi ya taaluma yao na kurudia kiapo chao ikiwa ni pamoja na kumkumbuka mwasisi wa uhuguzi duniani mama  france nightgiri aliyejitolea kufanya huduma hiyo kwa moyo na kujitoa bila ya kurudi nyuma.”kauli mbiu ya mwaka huu inasema “wauguzi nguvu ya mabadiliko uboreshaji wa uthabiti wa huduma ya afya”.

No comments:

Post a Comment