Tuesday 3 May 2016

PICHA:MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI YANAYOFANYIKA KITAIFA JIJINI MWANZA








Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Simon Berege, akitoa salamu za ufunguzi katika Maadhimisho ya Siku ya  Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016 yanayofanyika Kitaifa katika Hotel ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.


Katika Maadhimisho haya, litazinduliwa Chapisho la Uhuru wa Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika ambalo limeandaliwa na Misa Tanzania, chapicho hilo linaitwa "So This is Democracy"? (Je Hii ni Demokrasia).

Mgeni Rasmi katika Maadhimisho haya ni Jaji Mkuu wa Tanzania ambae amewakilishwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba. Pia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nhauye pamoja na Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Regnard Mengi wamehudhuria katika Maadhimisho haya.


Viongozi wengine wa Mashirika ya Kimataifa, Balozi mbalimbali, Taasisi Washirika, Wasomi wa Vyuo Vikuu pamoja na Wadau wengine wa habari wamehudhuria.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku hii kwa mwaka huu ni UHURU WA KUPATA HABARI YA NI HAKI YAKO.

No comments:

Post a Comment