Tuesday 10 May 2016

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROF. SOSPETER MUHONGO ATOA TAMKO KUHUSU KUACHIA MIAMBA TAKA (MAGWANGALA) MKOANI GEITA



Serikali imesema kuwa mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM)umekubali  kutoa miamba taka(magwangala) kwa ajili ya  wananchi mkoani hapa  hivyo  ni vyema kwa serikali ya mkoa kuhakikisha kuwa inatafuta  eneo kwa  ajili ya shughuli ya uchenjuaji.

Hayo yamesemwa na Waziri wa nishati na madini Prof.Sospeter Muhongo wakati  wa kikao na wachimbaji kilichofanyika katika ukumbi wa mkoa wa Geita,amesema kuwa swala la  magwangala mwisho wake  na majibu yake yatapatikana tarehe 30 ya mwezi wa sita  endapo eneo ambalo litapatikana litakuwa limekidhi vigezo na sheria  na kuwepo kwa usalama kwa eneo hilo.

Aidha  Waziri Muhongo ameutaka mgodi wa dhahabu (GGM)katika kikao cha  tarehe 30 kuhakikisha kuwa wanaonesha ni kiasi gani cha fedha walizotoa katika maendeleo ya mkoa kwa kipindi cha miaka mitano.


Kwa upande wao wabunge wa majimbo yote ya Geita waliokuwepo katika kikao hicho wametoa maoni yao tofauti juu ya kauli ya kutolewa kwa miamba taka tarehe 30 june.

No comments:

Post a Comment