Wednesday 11 May 2016

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA BUKOMBE AAGIZWA KUKOPA FEDHA KWA AJILI YA FIDIA KWA WANANCHI:GEITA

 
Baraza  la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe mkoani Geita limemwagiza mkurugenzi wa halmshauri hiyo James Ihunyo kukopa kiasi cha fedha cha sh,milioni 500 kwenye taasisi za kifedha kwa  ajili ya kulipa fidia kwa maeneo ambayo hayajapimwa hususani maeneo ya Uyovu na Namonge  ambayo  yanakua kwa kasi kubwa katika wilaya  hiyo.

Diwani wa kata ya Bulangwa Yusufu Mohamed,ametaka kujua kuwa yeye ni mjumbe wa kamati  ya ardhi lakini jambo ambalo limeendelea kuzua mjadala ,ni kwamba kamati  hiyo haijawai kukaa na kujadili juu ya changamoto  ambazo wananchi   wamekuwa wakikutana  nazo katika swala la upimaji wa ardhi.

Akijibu  swali  hilo mkurugenzi wa halmashauri  hiyo James Ihunyo,amesema kuwa  kamati hiyo kisheria inatakiwa kuwa na afisa ardhi mteule na kwa  sasa wilaya ya Bukombe haina afisa huyo hali ambayo imekuwa  ikisababisha kutokukaa  kwa kamati hiyo.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Safari Mayala,amesema kuwa hoja ya kukopa fedha kwa ajili ya kufidia ardhi  ni  hoja ya muda mrefu ambayo imedumu kwa muda wa miaka minne hali hiyo ndio iliyosababisha kumwagiza mkurugenzi kukopa ili waweze kufidia ardhi.

Aidha,mkurugenzi wa halmashauri hiyo ameongeza kuwa suala la kukope fedha kwa  ajili ya kulipa fidia kwa wananchi wanaendelea kushughulikia na  muda wowote wataanza kutoa fidia kwa wananchi ili waweze kuachia maeneo ambayo kuna uwezekano wa kuwekwa kwa miradi mikubwa.


No comments:

Post a Comment