Tuesday 17 May 2016

MBIO ZA MWENGE ZINATARAJIA KUFANYIKA JULY 30 WILAYANI BUKOMBE






































Wito umetolewa kwa watendaji wa kata na vijiji Wilayani Bukombe Mkoani Geita kuhakikisha wanahamasisha vikundi mbalimbali  vya burudani na Wananchi kujitokeza kushiriki mbio za Mwenge zinazotarajia kufanyika july 30 Wilayani humo
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa Kamati ya sherehe hizo ambae ni mkuu wa wilaya hiyo,mh amani mwenegoha wakati wa zoezi la kufanya tathimini na mapendekezo ya miradi itakayozinduliwa na kuwekewa jiwe la msingi wakati wa mbio hizo.

Awali mratibu wa mbio za Mwenge wilayani hapo, Elimkwasa John wakati akiwasilisha miradi iliyopendekezwa mbele ya viongozi na Wakuu wa idara mbalimbali .

Ameitaja miradi  iliyopendekezwa  ili  ijadiliwe na kufanyiwa maboresho na mapendekezo kuwa ni soko la wakulima wa mihogo kijijini Namonge,mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu katika shule ya sekondari Namonge , ujenzi wa Barabara ya Uyovu Kabagore na Kayenze pamoja na ukarabati wa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha Uyovu.


Aidha John amesema kuwa Mwenge unatarajia kuingia Wilayani Bukombe ukitokea Biharamlo mkoani Kagera ukibeba kauli mbiu isemayo vijana ni nguvu kazi ya taifa washirikishwe na kuwezeshwa .

No comments:

Post a Comment