Waziri wa
Madini,Bi Angellah Kairuki akiwa na Meneja wa Mgodi wa Buckreef Peter
Zishoo(Katikatika) na pembeni ni Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM)Mkoani
Geita Joseph Kasheku Msukuma wakati walipotembelea baadhi ya maeneo ya Mgodi
Huo.
Waziri wa
Madini,Bi Angellah Kairuki akiwa na mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya
ya Geita,Mwl Herman Kapufi wakati wa kikao na wabia wa mgodi wa Buckreef
alipotembea kwa lengo la kujadili namna ambavyo wanatakiwa kuanza kazi za
uchimbaji kwenye mgodi huo.
Mwenyekiti wa CCM
Mkoa wa Geita na Mbunge Joseph Kasheku Msukuma akiwa kwenye kikao hicho wakati
alipokuwa akichangia hoja ya fidia kwa wananchi wa kata ya Busanda na Kaseme.
Mjiolojia wa mgodi huo Bw Anthony Minde,akisisitiza
kutokuafikia swala la kuwalipa fidia baadhi ya wananchi.
Waziri wa
Madini,Bi Angellah Kairuki akisisitiza kupereka taarifa hiyo kwenye Wizara
ya ardhi kwaajili ya kutathimini kwa upya maeneo hayo.
Baadhi ya wajumbe waliokuwepo kwenye Kikao hicho.
Hatua hiyo imetokana na kutokuwepo kwa maelewano baina ya wabia wa Mgodi
huo ambao ni Kampuni ya Tanzam 2000 inayomiliki asilimia 55 huku asilimia
45 zikimilikiwa na shirika la madini nchini (STAMICO) waliogoma kulipa deni
hilo kutokana na kutokuwa na uhakika na madai hayo na kutokuwa na leseni.
Mjiolojia wa mgodi huo Bw Anthony Minde alisema hakukuwepo mgogoro wowote
kwani mkataba wa uthamini ulisainiwa na mkuu wa wilaya pamoja na aliyekuwa Mkuu
wa Mkoa wa Geita wakati huo, hivyo suala la kulipa fidia linakuwa gumu kwa
upande wao.
“Nafikiri waliosema kwamba walikuwepo ni kwamba Afisa wa Serikali na ni
wa Shinyanga, tuliletewa baada ya kuomba kwamba hii tathmini ifanywe na mtu wa
serikali ikaidhinishwa na kusainiwa kwenye ngazi ya wilaya na mkoa kabla ya
kuletwa kwetu ili tuisome kuona kama iko sawa, Tunamshangaa Mbunge anaposema
ripoti hiyo haikusainiwa” Alisema Minde.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoani
Geita Bw Joseph Msukuma aligoma kukubaliana na taarifa hiyo na kudai kuwa
walipeleka mthamini ambaye hakuripoti kwenye Halmashauri ya wilaya ya Geita na
kwamba walikuwa wakifanya uthamini huku wakiwanyang’anya marudio wananch.
“Walileta mthamini kutoka Shinyanga ambaye hakuripoti kwenye Halmashauri
ya wilaya ya Geita, ulipotokea mgogoro pale Kaseme tukaja, mlikuwa mnafanya
uthamini mnanyang’anya na marudio ya wananchi, ndo wananchi wakagoma
likasimamishwa hilo zoezi, huyo aliyekuja kurudisha kwenye ngazi ya Halmashauri
ni nani aliyeridhia? Na kama kweli mlifanya uthamini hawa asilimia mia moja
wametokea wapi?” Alisema Msukuma.
Waziri wa Madini Bi, Angellah Kairuki amechukua uamuzi wa kupeleka madia
hayo kwenye wizara ya ardhi na kwamba atamueleza Waziri husika kurudisha
wathamini wake kwa mara nyingine ili kujiridhisha kwa kila mwananchi kama
anaumiliki halali wa eneo analoliombea fidia.
“Sasa mimi uamuzi wangu ni kwamba, kama Serikali tutakaa tutalipeleka
suala hili wizara ya ardhi kupitia kwa waziri wa ardhi ili aelekeze wataalam
wake, wathamini wake tena kurudi kwenye jina moja baada ya jingine katika
majina hayo elfu moja na sitini na mbili kila mmoja kuweza kujiridhisha eneo
lake ni lipi na kama kweli ana umiliki nalo ili baada ya hapo sasa kama wao
walikuwa wamesema hawawezi kulipa kwa sababu hawana uhakika na orodha kamili
tutakuwa tumelimliza na wasipolipa tutakuwa tumejua nia yao sio nzuri” Alisema
Kairuki.
No comments:
Post a Comment