Katibu wa umoja wa wanawake wa chama cha mapiduzi wilayani Geita,Bi Mazoea Salum ,Akizungumza na kusisitiza wananchi kujitolea kuwasaidia watoto waishio mazingira magumu.
Wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia zoezi la utoaji wa msaada kwa watoto waishio mazingira magumu.
Uongozi wa Jumuiya ya wanawake wa chama cha mapinduzi wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wa Bright light pamoja na Mkurugenzi wa Kituo hicho.
PICHA NA JOEL MADUKA.
Jamii Mkoani
Geita imetakiwa kujitoa kwa moyo wa
kupenda kuendelea kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu na wale
ambao ni yatima.
Rai hiyo
ilitolewa na katibu wa umoja wa wanawake wa chama cha mapiduzi wilayani Geita,Bi Mazoea Salum wakati alipokuwa akiwakabidhi vifaa vya shule watoto
wa kituo cha kulea watoto cha Bright light kwenye kikao cha kwanza cha jumuiya
hiyo tangu uchaguzi kufanyika ndani ya chama.
Alisema kuwa
ni vyema jamii kwa ujumla kukumbuka kuwasaidia watoto ambao wana uhitaji kwani hata kwenye vitabu vya Mungu
vimeendelea kuelekeza kutoa msaada kwa yatima,wajane na wale ambao
hawajiwezi kwani kufanya hivyo ni kumpendaza Mungu.
Aidha kwa
upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho ,Methew Daniel ameelezea kuwa pamoja na
kuendelea kufanya vizuri kwenye kituo hicho bado wanakabiliwa na matatizo ya
jamiii kuendelea kukichukulia kituo hicho kuwa kina wafadhili jambo ambalo ni
kinyume na kituo kilivyo.
No comments:
Post a Comment