Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mke wa
Spika Bibi. Fatma Ndugai kwa niaba ya Spika Job Ndugai ikiwa ni cheti cha
utambuzi wa mchango wake katika kusimamia rasilimali za nchi hasa madini katika
hafla ya kuwatunuku vyeti wajumbe wa Kamati zilizohusika katika sakata la
Makinikia leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Katika ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
John Kijazi na Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi cheti
cha kutambua mchango wake katika kusimamia rasilimali za nchi mjumbe wa kamati
zilizoshughulikia masuala ya Makinikia ambaye pia ameteuliwa kuwa Gavana wa
Benki Kuu (BOT) Profesa Florens Luoga
wakati wa hafla ya kuwatunuku
vyeti wajumbe wa Kamati zilizohusika katika sakata la Makinikia leo Ikulu
Jijini Dar es Salaam. Katika ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi cheti
cha kutambua mchango wake katika kusimamia rasilimali za nchi mjumbe wa kamati
zilizoshughulikia masuala ya Makinikia Bibi. Monica Philip wakati wa
hafla ya kuwatunuku vyeti wajumbe wa Kamati zilizohusika katika sakata
la Makinikia leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) aliyeteuliwa
leo kushika wadifa huo Profesa Florens Luoga akisalimiana na Mufti na
Sheikh Mkuu wa Tanzania Juma Zuberi katika hafla ya kuwatunuku vyeti wajumbe wa
Kamati zilizohusika katika sakata la Makinikia leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Nyuma ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi William Lukuvi akisalimiana na
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Mussa Salum.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Haruna Lipumba walipokutana katika hafla ya kuwatunuku vyeti
wajumbe wa Kamati zilizohusika katika sakata la Makinikia leo Ikulu Jijini Dar
es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha
ya pamoja na baadhi ya Mawaziri na waliokuwa wajumbe wa Kamati zilizoshugulikia
suala la Makinikia wakati wa hafla ya
kuwatunuku vyeti wajumbe hao leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment