Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akisalimiana na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa Idara ya usalama wa chakula kwenye wizara hiyo Bi Josephine Amulo wakati alipowasili kwenye viwanja vya ccm kalangalala.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga,akipatiwa maelezo na mtaalum kutoka kwa wakala wa usambazaji wa mbegu wakati alipotembelea Banda hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwa kwenye moja kati ya mabanda ambayo yanahusika na uuzaji wa mbegu bora za kilimo.
Afisa uhusiano wa Tanesco Mkoa wa Geita Emma Nyaki akimuelezea kamanda wa jeshi la zima moto Mkoani Geita wakati alipotembelea banda ilo kwaajili ya kuona shughuli na utendaji kazi wa shirika la Tanesco Mkoani Humo.
Baadhi ya viongozi wa Wilaya wakitazama namna ambavyo jiko la kupikia la umeme linavyoweza kutumia umeme mdogo zaidi.
Afisa wa Tanesco Makao makuu Bi,Jennifer Mgendi akimuelezea Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga namna ambavyo wameendelea kutoa huduma kwa wananchi wakati alipo tembelea banda h la shirika hilo.
Mgeni Rasmi akipewa maelekezo ya namna ya kutumia kifaa endapo kama mteja akawa na nyumba ndogo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwa kwenye banda la TFDA.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwa kwenye banda la dawa zinazotokana na miti.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa Idara ya
usalama wa chakula kwenye wizara hiyo Bi Josephine Amulo akielezea umuhimu wa siku hiyo.
Mgeni Rasmi akimsikiliza kwa Makini Mwakilishi
wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa Idara ya
usalama wa chakula kwenye wizara hiyo Bi Josephine Amulo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi.
Wananchi wakiwa kwenye viwanja vya kalangalala wakifuatilia maadhimisho.
Brother K wa kikundi cha sanaa cha Futuhi akionesha makeke yake. PICHA NA JOEL MADUKA
Serikali
Mkoani Geita imeziagiza Halmashauri zote Mkoani humo kuendelea kupambana na
ukataji miti na uchomaji ovyo mistu ili kupunguza athari za kimazingira
zinazoathiri uzalishaji na upatikanaji wa chakula.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Chakula itakayoadhimishwa Kitaifa
mkoani Geita, Mkuu wa mkoa huo Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amesema ni
vema wakulima wakazingatia kilimo bora kwa kulima maeneo madogo ili kuboresha mazingira.
Mkuu huyo wa Mkoa ameendelea kuwasisitiza
wananchi kutumia fursa ya maonesho kwa ajili ya kujifunza mbinu mbalimbali za
kuendeleza sekta ya kilimo.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa Idara ya
usalama wa chakula kwenye wizara hiyo Bi Josephine Amulo ameelezea madhumuni ya
siku ya chakula duniani ni kuongeza ufanisi kwenye sekta ya kilimo.
Kaulimbiu ya
siku ya chakula duniani kwa mwaka huu ni, Badili Mwelekeo wa Uhamaji Wekeza
katika usalama wa chakula na Maendeleo Vijijini ambapo kilele cha maadhimisho
hayo ni Oktoba 16 mwaka huu na mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Kilimo Dr Charles
Tizeba.
No comments:
Post a Comment