Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro Bi. Siriel Mchembe akieleza mikakati iliyosaidia Wilaya hiyo kuongeza kiwango cha ufaulu hadi kufikia asilimia zaidi ya 70 mwaka huu kwa Shule za msingi wakati wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Walimu walipomtembelea Ofisini kwake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Tume
Afisa Utumishi wa Tume ya Utumishi wa Walimu Bi.
Anyagwe Lupembe akitoa ufafanuzi kuhusu taratibu sheria na Kanuni
zinazotumika katika utumishi wa Umma kwa watumishi wa Tume ya utumishi wa
Walimu Wilaya ya Gairo wakati wa ziara ya Ujumbe wa Tume
hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Tume ya utumishi wa Walimu Bi.
Devotha Gabriel akiwasiliosha mada kwa watumishi wa Tume hiyo Wilaya ya Gairo
kuhusu matumizi salama ya vifaa vya TEHAMA pamoja na njia sahihi za mawasilisno
kwa njia ya mtandao.
Mkuu wa Wilaya ya
Gairo Mkoani Morogoro Bi. Siriel Mchemba (katikati) akiwa kwenye picha ya
pamoja na Ujumbe wa Tume ya utumishi wa Walimu uliongozwa na Mkuu wa Kitengo
cha TEHAMA wa Tume ya Utumishi wa Walimu Bi. Devotha Gabriel. Wa kwanza kulia
ni Katibu Tawala wilaya ya Gairo Bw. Adam Bibangaba.
Wajumbe kutoka Tume ya
Utumishi wa Walimu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro Bi.
Siriel Mchemba wakati walipomtembelea Ofisini kwake.
(Picha zote na
Frank Mvungi- Gairo, Morogoro)
Akizungumza na
Makatibu Wasaidizi wa Wilaya wakati wa kuhitimisha ziara ya Wajumbe wa Tume
hiyo wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro, Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Devotha
Gabriel amewasisitiza viongozi hao kuzingatia taaluma ili waweze kutekeleza
majukumu yao kwa ufanisi.
“Mafunzo tunayowapa
Makatibu Wasaidizi katika Wilaya zote yanalenga kuwajengea uwezo wa kutumia
vifaa vya TEHAMA kwa kuzingatia sheria, kanuni pamoja na taratibu zote za
Utumishi wa Umma ikizingatiwa eneo mojawapo tunalosisitiza ni kufuata taratibu
za Utumishi wa Umma katika kuwahudumia walimu” Alisisitiza Devotha.
Bi. Devotha amesema
kuwa utaratibu wa kuwajengea uwezo watumishi wa Tume hiyo ngazi ya Wilaya ni
utekelezaji wa moja ya mikakati ya Tume hiyo ili kuongeza ufanisi katika
kuwahudumia walimu ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Aidha Bi. Devotha
alisistiza kuwa dhamira ya Tume hiyo ni kutekeleza maagizo yaliyotolewa hivi
karibuni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Selemani Jafo katika
kushughulikia masuala yote yanayowahusu walimu ndio maana Katibu wa Tume
amekuwa akifuatilia na kuhakikisha maagizo hayo yanatekelezwa kikamilifu.
Utekelezaji wa maagizo
ya Mhe. Wzairi unaenda Sambamba na kushughulikia masuala ya walimu kwa wakati
na kujenga mifumo ya TEHAMA ambayo inawaunganisha Makatibu Wasaidizi katika
ngazi ya Wilaya na Makao Makuu ya Tume hiyo hali itakayorahisha utendaji,
kupunguza gharama,kuokoa muda na kutua changamoto za walimu kwa wakati.
Aidha, Bi. Devotha
alitoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza na kusaidia juhudi za Tume ya
Utumishi wa Walimu katika kuimarisha utendaji kazi wa Tume hiyo kwa kujitolea
vifaa vya TEHAMA na kuwajengea uwezo Makatibu Wasaidizi ngazi
ya Wilaya.
Kwa upande wake mkuu
wa Wilaya hiyo Bi Bi Siriel Mchembe amesema kuwa Wilaya hiyo imefanikiwa kukuza
kiwango cha elimu hadi kufikia zaidi ya asilimia 70 ya ufaulu katika matokeo ya
Darasa la saba.
“Nimefanikiwa
kusimamia kikamilifu ujenzi wa miundo mbinu kama madarasa, vyoo na miundo mbinu
mingine hali ambayo imeongeza na kukuza morali ya walimu katika Wilaya yetu.”
Alisisitiza Mchembe.
Akifafanua Mchembe
amesema maendeleo ya sekta ya elimu katika Wilaya yake ni Kipaumbele na ameweka
utaratibu mzuri wa kusimia utekelezaji wa mikakati ya kukuza elimu Wilayani
humo.
Kwa upande
wake Afisa Utumishi wa Tume hiyo Bi Anyagwe Lupembe amesema kuwa
Tume hiyo imejikita kujenga uwezo kwa watumishi wake ili watimize majukumu yao
kwa kuzingatia sheria Kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.
Tume ya Utumishi wa
Walimu imekuwa ikitekelza mpango wa kuwajengea uwezo Makatibu wasaidizi katika
Wilaya zote nchini na kwa kuanza tayari mpango huo umetekelzwa katika mikoa ya
Dodoma na Morogoro hivyo ni muda muafaka kwa wadau kujitokeza kuunga mkono
juhudi hizo.
No comments:
Post a Comment