Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Lughumbi akisalimiana na watumishi pamoja na wakuu wa idara mbali mbali Mkoani humo. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Lughumbi akimkabidhi hati ya pongezi Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye kwasasa amestaafu Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye kwasasa amestaafu Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akionesha Hati ya pongezi ambayo amepatiwa na Mkoa wa Geita wakati alipokuwa akiagana na watumishi. |
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye kwasasa amestaafu Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akimkabidhi Mkuu wa Mkoa mambo muhimu ambayo ameyaandika wakati wa hafla ya kukabidhiana ofisi. |
Wakuu wa Wilaya wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa huo pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi(CCM). |
Mkuu wa Mkoa wa Geita akiwa kwenye ofisi yake kwaajili ya kuanza shughuli rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Lughumbi
amewataka watumishi na wakuu wa wilaya Mkoani humo kuwatumikia kikamilifu
wananchi wenye matarajio makubwa kwa serikali yao.
Mhandisi Lughumbi aliyasema hayo alipozungumza na watumishi
na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo katika hafla ya kukabidhiwa ofisi na
Mtangulizi wake Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga aliyestaafu nafasi hiyo.
Alisema amefika kwenye Mkoa wa Geita kufanya kazi hivyo watumishi wote
wawajibike kuchochea maendeleo kwa kasi ikiwemo kuboresha miundombinu ya elimu.
“Nimeingia katika Mkoa huu kama
mlivyonikaribisha mmenikaribisha nimekuja kufanya kazi nimekuja kutumika
nimetumwa kuwa mtumishi kwa mwendo tulionao hatuna muda wa kupumzika ni kipindi
cha mageuzi lazima tugeuze kitu kigeuzike watu wajue tumegeuza hata
wanaofuatilie waone mambo yapo sawa sawa ukione maendeleo yanakimbia ujue
uku kulipokuwa kunachelewa vilikuwa vipindi vigumu vya matengenezo”
Alisema Lughumbi.
Pia amezungumzia tatizo la uduni wa miundombinu ya elimu na shida ya maji
inayoendelea kuwasumbua wananchi wa Geita.
“Wakina mama bado wanandoo kichwani
katika Mkoa tupo asilimia hamsini upatikanaji wa maji safi na
salama kuna watu wamecheza na fedha ya umma maji hayajaja tangu
miaka ya sabini meja jenerali wewe ulikuwa mpole mimi naenda kwenye sait
nitakuwa mkali kidogo hasa ambao wanacheza na mali ya umma” Alisisitiza Lughumbi.
Mkuu wa Mkoa mstaafu, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga alisema kwa
sasa anakwenda kupumzika na kuwataka wanaobaki kulitumikia taifa wafanye kazi
kwa weledi na kasi inayoendana na ile ya Rais Dkt. John Magufuli.
Mkoa wa Geita ni Kati ya Mikoa ambayo ilianzishwa mwaka 2012,na wakuu wa
Mikoa ambao wamepita hadi sasa ni watatu, Said Magalula, Fatuma Mwasa na Meja
jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ambaye amestaafu hivi karibuni na kumpisha Mhandisi
Robert Lughumbi.
No comments:
Post a Comment