Mabomba
ambayo yanatoka kwenye mradi wa Nchakolongo yakiwa yametandazwa wakati Mkuu wa
Wilaya ya Geita alipokwenda kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi
pamoja na wataalam.
Chanzo
cha maji ambacho ndio kinatumiwa na wanakijiji wa kijiji cha Chikobe.
Mkuu wa
Wilaya ya Geita ,Mwl Herma Kapufi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chikobe
juu ya hatua ambazo zinaendelea kutekelezwa na serikali ili kumaliza mradi huo
na tatizo la maji kwenye kijiji hicho.
Wakizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara baadhi ya wananchi
hao Bi Pili Simon Goi na Maganga Paul Walisema kuwa wamekuwa wakitumia muda
mrefu kutafuta maji na kwamba kumekuwa na mabomba yanayowekwa bila kutoa maji
huku kukiwa na mradi wa maji ulioanza mwaka (2010 )lakini haujakamilika hadi
sasa.
“Sisi wakina mama ndio wahanga wakubwa ukosekanaji wa maji
kwani tumekuwa tukiamka usiku wa manane kwenda kutafuta maji na muda mwingine
tunakuwa na hofu kubwa kutokana na kuogopa kufanyiwa vitendo vya ukatili
likiwemo swala la kubakwa kwakweli tunatesekan Sana”Alisema Bi,Pili Goi.
“Kuna mradi ambao umeanzishwa tangu mwaka 2010 lakini jambo la
kusikitisha hadi sasa mradi huo ujakamilika na tunapata shida ya maji tunaomba
serikali itusaidie juu ya swala hili”Alisema Maganga Paul.
Akizungumza kwenye Mkutano huo wa hadhara Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl
Herman Kapufi aliwataka wakazi wa kijiji hicho kuwa wavumilivu kwa kuwa tatizo
hilo litapatiwa ufumbuzi muda mfupi ujao.
Kaimu mhandisi wa maji wa Wilaya ya Geita Bw Yusuf Chalamanda
alisema mradi wa maji wa Nchankolongo umechukua muda mrefu kutokana na tatizo
la fedha na baadhi ya wakandarasi kutokuwa waaminifu na
kwamba wanatarajia kuanza kufanya majaribio kwa kusambaza
maji kwenye vijiji vya Chikobe, Nchankolongo, Chiguga na Kabayozo na pia mradi
huo utakamilika na kuanza kusambaza maji rasmi Desemba 12 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment