Afisa
mahusiano Mkuu katika Benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) Ndg
Saidi Mkabakuli (Kushoto) akimkabidhi baadhi ya vipeperushi Katibu Mkuu
wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Methew Mtigumwe (Kulia) wakati alipotembelea banda la Benki
hiyo kwenye maadhimisho
ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa katika viwanja vya kalangalala
Mkoani Geita.
Meneja Mwendeshaji wakulima wadogo katika Benki ya Maendeleo
ya kilimo Tanzania (TADB) Ndg Joseph Mabula (Kulia) akitoa maelezo ya namna wanavyofanya kazi mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Methew Mtigumwe (Kushoto) wakati alipotembelea banda la Benki
hiyo kwenye maadhimisho
ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa katika viwanja vya kalangalala
Mkoani Geita.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Methew Mtigumwe akisikiliza maelezo kutoka kwa afisa wa shirika
la chakula Duniani (FAO) na Programu ya Chakula duniani (WFP) wakati alipotembelea banda la shirika hilo kwenye maadhimisho
ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa katika viwanja vya kalangalala
Mkoani Geita
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Kilimo
Mhandisi Methew Mtigumwe akisikiliza maelezo kutoka kwa Msaidizi wa Mawasiliano wa Utafiti katika Taasisi ya
Kimataifa ya Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) nchini Tanzania Bi
Eveline Massam wakati alipotembelea banda la shirika hilo kwenye maadhimisho
ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa katika viwanja vya kalangalala
Mkoani Geita
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Kilimo
Mhandisi Methew Mtigumwe akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa wa Utafiti katika Taasisi ya
Kimataifa ya Kilimo ukanda wa Kitropiki (IITA) nchini Tanzania wakati alipotembelea banda la shirika hilo kwenye maadhimisho
ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika viwanja vya kalangalala
Mkoani Geita
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Methew Mtigumwe wakati alipotembelea banda la Benki hiyo kwenye maadhimisho
ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanataraji kufika ukomo Kesho Octoba
16, 2017 kwenye viwanja vya kalangalala Mkoani Geita.
Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa ufinyu mkubwa wa
upatikanaji wa fedha za mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini unachangiwa
kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka Taasisi za fedha kuelekezwa zaidi
kwenye upande wa biashara za bidhaa, riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo, Mikopo
ya muda mfupi, masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta
ya kilimo na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali
ya hewa.
Alisema kuwa kupitia changamoto hizo serikali
imeamua kuanzisha Benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia
kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya
kilimo ili kuleta mapinduzi katika kilimo nchini.
Mhandisi Mtigumwe alisema kuwa miongoni mwa
madhumuni makubwa ya kuanzishwa kwa Benki hiyo ni pamoja na kusaidia
upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini pamoja
na kuchagiza na kusaidia mapinduzi ya kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda
kilimo cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza
umasikini.
Kwa upande wake Meneja Mwendeshaji wakulima wadogo kutoka
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Ndg Joseph Mabula alisema kuwa
pamoja na mambo mengine pia Benki hiyo imedhamiria na kujidhatiti kuhakikisha
inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta Mapinduzi yenye tija katika sekta ya
kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja na
sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini.
Mabula aliongeza kuwa malengo mkakati ya Benki hiyo
ni kuinua uzalishaji wenye tija katika sekta ya kilimo kwa kuendeleza miundombinu
muhimu, mathalani, Skimu za umwagiliaji, Usafirishaji, Hifadhi ya Mazao, Usindikaji
na Masoko.
No comments:
Post a Comment