Mwenyekiti wa chama cha waandishi Mkoani
Geita,Daniel Limbe Akisisitiza Msimamo wa waandishi wa habari wakati wa kikao
cha
Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza
Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa Habari Mkoani Humo wakati wa kikao cha
maadhimio
Baadhi ya waandishi wa Habari Mkoani Geita wakiwa
kwenye picha ya pamoja nje ya ofisi hizo.
Uamuzi huo umefikiwa leo baada ya kumalizika kikao cha dharula cha
waandishi wa habari ambao walikutana ili kujadiliana namna bora ya kukabiliana
na unyanyasaji unaofanywa na jeshi la polisi kwa waandishi wa habari mkoani
Geita.
Tamko la kuondoa ushirikiano kwa jeshi la polisi limesomwa na mwenyekiti
wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita Daniel Limbe (pichani),ambaye
amesema uamuzi huo utatenguliwa iwapo uongozi wa Jeshi la polisi mkoani humo
utajitokeza kuomba radhi kwa vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na polisi
pamoja na kuwahakikishia usalama wao wawapo kazini.
Aidha uamuzi huo umeanza kutekelezwa baada ya tamko hilo huku ikielezwa
kuwa mwandishi wa habari atakayekiuka makubaliano hayo atachukuliwa hatua zaidi
ikiwa ni pamoja na kufutwa uanachama wake ndani ya Klabu hiyo.
Uamuzi huo umekuja ikiwa ni siku mbili zimepita tangu waandishi wa habari
wanne kushambuliwa na kuharibiwa vifaa vya kazi wakati wakichukua matukio ya
vurugu zilizotokea kwenye shule ya sekondari Geita(Geseco) ambayo pia wanafunzi
walikuwa wakitishia kuichoma moto iwapo wenzao watano waliokuwa wanashikiliwa
na jeshi la polisi hawataachiliwa huru na kulejea shuleni hapo.
Waandishi waliokutana na masaibu hayo na vyombo vyao kwenye mabano ni
Editor Edward(Mtanzania),Rehema Matowo(Mwananchi),Ester Sumira(Azam Tv) na
Emmanuel Ibrahimu(Clouds tv).
No comments:
Post a Comment