Mkoa wa Geita unakabiliwa na
upungufu wa walimu elfu 13 na 577 huku waliopo wakiwa elfu 8 na 568 wa shule za
msingi mkoani humo hali inayosababisha uwiano kati ya walimu na wanafunzi
kushuka kuanzia Mwaka 2013 hadi sasa
Imeelezwa kuwa wanafunzi 31 wa
shule za msingi na 196 wa Sekondari wamekatisha masomo baada ya kupata ujauzito
kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 mpaka sasa.
Akisoma taarifa ya maendeleo ya
Elimu Mkoani Geita katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Elimu ngazi ya
Mkoa, Afisa Elimu Mkoani humo Rehema Mbwilo amesema wilaya yenye upungufu
mkubwa wa walimu ni Bukombe yenye upungufu wa asilimia 49
Kaimu Katibu tawala wa Mkoa huo Bw
Emily Kasagala amewasisitiza wanafunzi kupenda Elimu na kuachana na utoro unaoweza
kusababisha kuzorta kwa viwango vyao kitaaluma
Baadhi ya wanafunzi mkoani Geita
Loveness Majaliwa na Rehema Joseph
wameiomba serikali kutatua changamoto za kielimu zilizopo ili wawe na
mazingira mazuri ya kujifunzia huku kaimu mkuu wa mkoa wa Geita Bw Herman
Kapufi akiahidi kushughulikia changamoto hizo.
No comments:
Post a Comment