Jeshi la Polisi katika
Mji wa Kisumu, nchini Kenya limelazimika kuanza kutumia nguvu kuwatawanya kundi
la vijana waliojitokeza mtaani kuanza kuchoma matairi ya magari, wakidai
kuibiwa kura kwa mgombea wao wa urais anayeungwa mkono na Muungano wa Nasa,
Raila Odinga.
Tukio hilo limetokea
baada ya saa chache Odinga kujitokeza mbele ya vyombo vya habari akituhumu
uchakachuaji wa kura zake uliofanywa na Tume ya Uchaguzi isiyokuwa na mipaka
(IEBC) wakati wa tukio la kuhesabu kura.
Wananchi nchini Kenya
walipiga kura katika Uchaguzi Mkuu siku ya jana ,kabla ya vituo hiyo kufungwa
kuanzia saa 11:00 jioni.
Polisi walilazimika
kutumia nguvu huku wakirusha risasi hewani ili kuwatawanya.
Baadaye Polisi iliamua
kuondoa mawe yaliyokuwa yametegwa na vijana hao barabarani.
Katika hatua nyingine,
kuna taarifa za kupigana kwa wafuasi wa wagombea ubunge katika kituo vha
kujumlishia matokeo , kilichopo Mji wa Mokewe, uliopo Lamu kabla ya Polisi
kuwasili eneo la tukio na kurejesha hali ya utulivu
No comments:
Post a Comment