Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu akiwa ameshikilia
vifaa vya kuchomelea vyuma kuashiria kuanza kuweka msingi wa kivuko ‘’Keel
Laying’’ katika eneo la Pasiansi ikiwa ni kumbukumbu ya kuanza rasmi kwa ujenzi
wa kivuko kipya kitakachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza.
Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na
utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu akichomelea vyuma
kuashiria kuweka msingi wa kivuko ‘’Keel Laying’’ katika eneo la Pasiansi ikiwa
ni kumbukumbu ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma
kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika
ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.
Meneja
wa Miradi wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya
Jijini Mwanza Major Songoro (kushoto) akitoa maelezo kwa Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kulia) kuhusu kuanza kwa
mradi wa ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa
kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya
shilingi Bilioni 8.9.
Meneja
wa Miradi wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya
Jijini Mwanza Major Songoro (kulia) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto) michoro itakayotumika
katika Ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa
kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya
shilingi Bilioni 8.9.
Meneja
wa miradi wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya
Jijini Mwanza Major Songoro (kulia) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (katikati) michoro itakayotumika
katika Ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Songoro Bwana Salehe Songoro. Ujenzi wa
kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya
shilingi Bilioni 8.9.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya
Jijini Mwanza Bwana Salehe Songoro (wa
pili kulia aliyenyoosha mkono) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (wa tatu kushoto) mojawapo ya malighafi
itakayotumika katika ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi. Ujenzi wa
kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya
shilingi Bilioni 8.9.
Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu, ameshiriki katika zoezi
la kuweka msingi wa ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma ya usafiri katika
Ziwa Victoria kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Zoezi hilo linaloashiria kuanza rasmi kwa ujenzi huo limefanyika
Pasiansi katika eneo linalotumika kwa ajili ya ujenzi wa meli, vivuko na boti
linalomilikiwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Limited ya Mwanza
iliyoshinda zabuni ya kujenga kivuko hicho kwa gharama ya Shilingi Bilioni 8.9
za kitanzania. Tukio hili la kihistoria lilihudhuriwa
pia na Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko kutoka TEMESA
Mhandisi Japhet Y. Maselle, Mhandisi Amos Mutahiwa kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Bwana Salehe Songoro Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro,
na wafanyakazi wa Kampuni ya Songoro na wale wa TEMESA.
Akiongea baada ya
zoezi hilo, Dkt. Mgwatu amesema wakazi wa Mwanza wana kila sababu ya kujivunia
kuanza kwa ujenzi wa kivuko hicho kwani kitakapokamilika kitasaidia kurahisisha
usafiri wa abiria na mali zao na hivyo kuimarisha uchumi wao. Aidha Dk. Mgwatu amemtaka
Mkandarasi kuhakikisha anamaliza kujenga kivuko ndani ya muda uliopangwa kwenye
mkataba na kuzingatia ubora wa hali ya juu. Pia ameishukuru Serikali kwa
kuendelea kutenga fedha za maendeleo kwa ajili ya miradi ya vivuko kwa lengo la
kuboresha huduma za usafiri. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro ameahidi
kukamilisha mradi huo kwa wakati huku akisisitiza kuwa kampuni yake imejipanga
vyema kufanya kazi kwa kasi kwa kuwa malighafi kwa ajili ya ujenzi wa kivuko
tayari ipo kwenye eneo la ujenzi.
Kivuko hicho kipya
kitakapokamilika kitafanya idadi ya vivuko vinavyotoa huduma katika eneo la
Kigongo Busisi kufikia vinne vikiwemo vile vya MV. Sengerema, MV. Misungwi,
pamoja na MV. Sabasaba.
No comments:
Post a Comment