Serikali
imesema kuwa viwanda vingine 42 vitaunganishwa na mfumo wa matumizi wa matunizi
ya gesi asilia katika kipindi cha miaka miwili ili kuongeza tija tofauti
viwanda 37 vya sasa ambavyo tayari vinatumia gesi hiyo.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani aliiambia Kamati ya Fedha ya
Bunge jana kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa changamoto zinazokwaza
zoezi la kuvipatia viwanda nishati hiyo zinatatuliwa haraka.
“Tuna
gesi ya kutosha futi za ujazo trilioni 57.25 ambapo hadi sasa tunatumia wastani
wa futi za ujazo milioni 70 ikiwa ni kama asilimia kumi tu hivi” alieleza
Waziri Kalemani
Kwa
hivyo alisema azma ya Serikali ni kuona viwanda vinatumia gesi katika
uzalishaji na kubanisha kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwa na nishati hiyo katika
Afrika Mashariki.
Waziri
Kalemani aliieleza kamati hiyo kuwa hivi sasa wateja wakubwa wa gesi hiyo ni
viwanda lakini Serikali ipo mbioni kutekeleza mkakati wa kusambaza gesi hiyo
kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Katika
maelezo yake kwa kamati hiyo ambayo ilitembelea kituo cha kupokelea gesi asilia
huko Kinyerezi na miradi ya uzalishaji umeme kwa kutumia gesi hiyo ya Kinyerezi
I na Kinyerezi II, Naibu Waziri huyo alidokeza
kuwa Serikali ina mpango wa kuanzisha kiwanda cha kusindika gesi asilia ili
iweze kusafirishwa nchi za nje.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Bunge Hawa Ghasia ameitaka TPDC kutayarisha
mpango maalum kwa kuainisha na kutenga maeneo maalum ambayo yatawekewa
miundombinu ya gesi ili uwekezaji wa viwanda uzingatie ramani hiyo.
“Tungetengeneza
kanda maalum tukaziandaa kwa ajili ya viwanda kwa kuziwekea miundombinu ya gesi
tofauti na sasa ambapo serikali inalazimika kuvifuata viwanda viliko
kuvipelekea nishati hiyo” alishauri Mwenyekiti huyo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti huyo
alieleza kuwa shirika hilo lina nafasi ya pekee katika kuifanya Tanzania
kufikia lengo lake la kuwa nchi ya viwanda kama itatekeleza vyema miradi ya
matumizi ya gesi viwandani.
Aliueleza
uongozi wa TPDC na waandishi wa habari walioambatana katika ziara hiyo kuwa madhumuni
ya ziara ya kamati yake katika miradi hiyo ni kuangalia utayari wa shirika hilo
katika kuchangia maendeleo ya uchumi wa viwanda bila ya vikwazo.
Mwenyekiti
huyo alieleza kuwa kamati yake imeridhika na kazi inayofanyika hadi sasa na
kueleza matumiani ya kamati yake kuwa miradi ya Kinyerezi I na Kinyerezi II
itamalizika kwa wakati na kufikia malengo yaliyowekwa.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Mhandisi Kapulya Musomba mpango wa
shirika lake sasa ni kutekeleza programu yake ya kusambza gesi nchi nzima kwa
kuanzia na mikoa ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Tanga.
Alisema
shirika lake lipo tayari kukipatia kiwanda au mwekezaji nishati hiyo katika
sehemu yeyote ambayo bomba la gesi hiyo limepita na kwamba ingependeza kuona
Tanzania ina viwanda vingi ili gesi yote iweze kutumika humu nchini pasi na
kusafirishwa nchi za nje.
Mapema
akijibu maswali kutoka kwa wajumbe wa Kamati hiyo, Mhandisi Musomba alisema
shirika lake linatumia mifumo miwili ya usalama wa bomba lenye urefu wa
kilomita 551 linalosafirisha gesi kutoka Mtwara hadi eneo hilo.
Aliitaja
kuwa ni mfumo unaojitegemea wa bomba hilo ambapo zinapotokea hitilafu hujizima
na wataalamu hufuatilia kuelewa hitilafu iliopo na mfumo wa pili ni ulinzi
shirikishi ambao wanawatumia wananchi kulinda bomba hilo.
Mbali
na viwanda 37 kuunganishwa katika mfumo wa matumizi ya gesi, shirika hilo pia
limeziunganisha familia 70 katika mfumo wa matumizi ya gesi hiyo katika maeneo
ya Mikocheni jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment