Kiongozi wa
Mbio za Mwenge wa uhuru ,Amour Hamad Amour pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Geita
,Mwl Herman Kapufi wakikagua mtambo wa kuchakata Alizeti.
Kiongozi wa
Mbio za Mwenge wa uhuru ,Amour Hamad Amour akiweka Mbigu za Alizeti kwenye
mashine ya kuchakata.
Ubao
unaonesha kikundi kilipo.
Vikundi vya wajasiriamali Wadogo wadogo bado vinakabiliwa na changamoto
mbali mbali likiwemo swala la kukosekana kwa vifungashio vya bidhaa ambazo
wamekuwa wakizitengeneza kwaajili ya kuingiza Sokoni Hali ambayo inapelekea
kushuka kwa thamani Bidhaa ambazo wanaingiza Sokoni.
Hayo yametokea wakati wa uzinduzi wa mradi wa kukamua na kusindika
mafuta ya alizeti cha Chemamba wilayani Geita ambapo wanakikundi cha
ujasiriamali wamekuwa wakikusanya chupa ambazo zimekwisha kutumika na kuwekea
mafuta na pia rebo wamekuwa wakitumia kwa kuandika kwa Mkono na sio zile ambazo
zinakuwa zinatambulisha shughuli za kikundi pamoja na namba za simu za
wahusika.
Kutokana na hali ambayo wamekutwa nayo wanakikundi hao na Kiongozi wa
mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour imemlazimu kuagiza Halmashauri
husika kukikopesha kikundi hicho fedha ambazo zitawasaidia katika kuboresha
shughuli ambazo wanazifanya.
Akisoma risala na taarifa ya Mradi Huo kwa Kiongozi wa
mbio za mwenge uhuru Afisa kilimo wa halmashauri ya wilaya ya
Geita Jeremia Kengere amesema uwepo wa mradi huo umehamasisha
wananchi kujikita kulima zao hilo la alizeti kwani wengi wao wamenufaika
kutokana na kilimo hicho.
Mkuu wa Wilaya hiyo,Mwl Herman Kapufi ameitaka halmashauri husika
kuhakikisha wanakipa kipa umbele kikundi hicho kwa kukiwezesha Mkopo ambao
utawasaidia kujikwamua Hali ambayo wanayo kwasasa.
Mwenge wa uhuru umezindua na kutembelea na kuweka jiwe la msingi
miradi Kumi Na Moja na kukibizwa wilaya ya Nyangh'wale.
No comments:
Post a Comment