Wakuu wa Wilaya zilizopo Mkoani Geita pamoja na
wabunge na wadau wa Kilimo cha Pamba wakifuatilia kwa makini Mkutano huo
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Bukombe ,Dionis Myinga akijitambulisha mbele ya wadau wa sekta ya kilimo cha
pamba.
Mkuu wa Mkoa
wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza kwenye mkutano
wa wadau wa kilimo cha pamba
Zao la biashara la pamba ni moja kati ya muhimili mkubwa wa uchumi nchini
na katika Mkoa wa Geita lakini kwa miaka ya hivi karibuni limeendelea kupoteza
umaarufu kutokana na mbegu kutokuwa na ubora pamoja na viuatilifu na bei
kutokuwa na mpangilio.
Hali hii ndio inayosababisha wadau wa pamba wakiwemo Viongozi wa
Wilaya,Wabunge ,maafisa Kilimo,washauri na wakulima kukutana kwenye ukumbi wa
ofisi za Mkuu wa mkoa wa Geita kujadili namna wanavyoweza kuendelea kuinua
kilimo cha pamba ili kuwa na faida kwa mkulima na mnunuzi.
Katika Mkutano huo Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja
Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amesisitiza kwa wadau wa kilimo cha pamba kuwa
kila mmoja anawajibu wa kuhakikisha kuwa kilimo hicho kinarudi na kinafufuliwa
katika ubora wake uliokuwepo miaka ya nyuma.
“Tunawajibu wa kuhakikisha kwamba kilimo hiki kinarudi kwenye ubora wake
na hakuna kinachoshindikana ni sisi kujipanga vizuri ikiwa ni pamoja na kurejea
historia kwani itatusaidia”Alisema Kyunga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe,Safari Nicas
Mayala,ameelezea sababu za zao la pamba kuanguka ni kukosa mtu anayeweza
kuhudumia na kwamba zamani vyama vya ushirika vilikuwa makini katika usambazaji
wa mbegu zenye uhakika.
“Pamba imeanguka baada ya kukosa mtu wa kuihudumia, mtu wa kuhihudumia
alikuwa ni ushirika vyama vya ushirika hadi miaka ya 1990, sasa hivi wangekuwa
wamesambaza mbegu ya pamba na dawa na Siyodani na ndio maana hapa mkulima
amesema kwamba turudishie Siyodani namba 25 ilikuwa inafanya kazi vizuri licha
ya kupingwa marufuku kutokana na uharibifu wa mazingira”Alisisitiza Mayala.
Akifunga Mkutano huo Mkuu wa Mkoa Ezekiel Kyunga,amesisitiza kuwa suala
la umoja wa wanunuzi wa zao la Pamba, UMWAPA halipo kwani walipatiwa ridhaa ya
mwaka mmoja kama majaribio na Waziri ambaye alikuwa madarakani kwa miaka hiyo
na kwamba walipatiwa wafanye kazi kwa majaribio kwa mwaka mmoja na
wameshapatiwa maelekezo ya kutowakandamiza wakulima kupitia UMWAPA.
No comments:
Post a Comment