Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto imekutana na wadau wa masula ya jinsia mkoani Dodoma wanaokutana
kudurusu Sera ya Mendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 ili kuiboresha
kwa kuzingatia mazingira na mahitaji ya sasa.
Akifungua kikao hicho Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Bibi Sihaba alisema kuwa
ushiriki wa wadau kutoka ngazi ya Halmashauri ni wa muhimu ili kuibua maoni ya
wananchi yatakayosaidia kuboresha sera iliyopo ili kuweza kuzingatia changamoto
zinazowakabili wanawake katika maeneo ya mijini na vijijini ili kufanikisha
azama ya Taifa ya kuwa na maendeleo endelevu kwa wanawake hapa nchini.
“Nyinyi ni Wadau muhimu na ndio mnaosimamia
utekelezaji wa Sera na mkikakati ya Sera katika ngazi ya mkoa na Halmashauri
maoni na changamoto mnanazotukutana nazo ni muhimu ili kujumuisha katika
kipindi hiki cha kuhuisha Sera hii” alisema Bibi Sihaba.
Akiongea katika kuwasilisha mada elekezi, Mtaalamu
Mwezeshaji Prof. Linda Mhando amesema Sera pendekezi itawezesha kufanya tathimi
itakayotoa mwelekeo kuona kuwa mipango na mkakati mbalimbali inazingatia mambo
muhimu yanayohimiza jamii kuachana na mitazamo ya kuwatambua wanawake peke yao,
na badala yake kutambua ushiriki wa wanaume kama wadau muhimu katika Sera hii.
Pro Linda, aliongeza kuwa Sera inayopendekezwa
itahimiza ushiriki sawa wa wanawake katika ngazi za uongozi na maamuzi,
upatikanaji wa haki sawa kwa wanawake, uwepo wa hifadhi za jamii, kupunguza
mzigo wa kazi, kuwashirikisha wanawake katika shughuli za kiuchumi na
kuwahusisha wanawake katika fursa mbalimbali ili kufikia malengo ya maendeleo
endelevu.
Akizungumaza katika kikao hicho Bi. Dafrosa Sanga
Mchumi Wizara ya Maliasili na Utalii alibainisha kuwa sera hii iwanufaishe
wavulana na wasichana, wanawake na wanaume kwani hivi sasa watoto wengi wa
kiume ndio wanaoathiriwa zaidi na utoro shuleni na maisha ya mitaani
ukilinganisha na watoto wa kike. Wadau wameipongeza Wizara kwa uamauzi wake wa
kuwashiriukisha wadau wa ngazi zote ili kupanua wigo wa maoni katoka ngazi
mbali mabli kwa ajili ya umiliki wa sera hiyo na uzingatiaji wa haki kijinsia.
Maoni ya wadau yatakuwa msingi wa kuboresha Sera
iliyopo ili kuimarisha uandaaji wa sera inayokidhi upatikanaji wa haki za
wanawake na wanaume katika ngazi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment