Friday 28 July 2017

UZINDUZI WA FILAMU YA MAGWANGALA WAINGIA DOSARI


Meneja Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Geita,Manase Ndoroma akielezea kutokuwepo kwa ugomvi wa aina yoyote kati ya wasanii na mgodi wa GGM na hatua ambayo wameichukua baada ya kuonekana kuwepo kwa mahudhui ambayo yanaleta uchochezi baina ya wananchi na mgodi.


Mwenyekiti wa chama cha wasanii Mkoani Humo ambaye pia ni moja kati ya wachezaji wa Filamu Hiyo ,Bi,Rosemery Michael(Rose Bonanza )Akielezea namna ambavyo wameweza kuingia hasara kutokana na uwandaaji wa filamu pamoja na uzinduzi.


 Naibu Waziri wa Habari Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura.Akizungumza juu ya kukwama kwa uzinduzi wa Filamu ya Magwangala ambayo imechezewa Mkoani Geita na wasanii pamoja na viongozi wa Serikali. 
Uzinduzi wa Filamu ya Magwangala  ambayo imechezwa na wasanii wa Mkoani  Geita pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Mji   ulikuwa ufanyike siku jana (Julai 27) umekwama kutokana na kuwepo kwa madai ya mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) Kulalamika kuwa filamu hiyo inaonekana kuwa na mahudhui ya  uchochezi baina ya wananchi na mgodi Mkoani humo.

Uzinduzi  huo ulitarajia kufanywa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura Katika ukumbi wa Desire Park .

Akizungumza  juu ya hatua ya kukwama  kwa uzinduzi huo Naibu waziri 
Wambura,amesema kuwa kilichotokea alipatiwa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa kwamba kuna picha ambayo sio nzuri na kwamba wao kama mgodi walilalamika juu ya picha hiyo na kwamba wameangalia na kuona kuwa kuna maeneo ambayo yamerekodiwa sio mazuri na tatizo ni mawasiliano baina ya Afisa utamaduni na Mkoa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wasanii  Mkoani Humo ambaye pia ni moja kati ya wachezaji wa Filamu Hiyo  Bi,Rosemery Michael ,amesema kuwa wao hawakuona mapungufu yoyote kwa maigizo ambayo wameigiza kwenye filamu hiyo ni uhalisia wa maisha ambayo yapo ndani ya Mkoa usika.

Baadhi ya wasanii na wananchi ambao wameudhuria siku ya jana kwenye uzinduzi wa Filamu Hiyo,Sagari Mganga na Neema Philipo wamesema kuwa hata wao wameshindwa kujua ni maswahibu gani ambayo yamejitokeza ambayo yamesababishwa filamu hiyo kutokuzinduliwa.

Manase Ndoroma ni meneja mwandamizi wa mgodi  ambaye anashughulika na maswala ya jamii, ndani ya Mgodi wa dhahabu wa Geita  (GGM)  amefafanua kuwa wao  hawana ugomvi na sanaa wala na wasanii ila kumetokea shida ambayo wametoa kwa jamii kwa makusudi na kwamba mgodi huo una athari kwa jamii ambayo inauzunguka.

No comments:

Post a Comment