Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema katika
wakati wake hakuna kupata pesa kwa njia rahisi kwani lazima ufanye kazi kweli
ili kupata pesa halali.
Rais Magufuli amesema
hayo leo Handeni wakati anaelekea mkoani Tanga kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la
msingi mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka
Chongoleani Tanga. Utaofanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 05 Agusti mwaka huu.
"Kuna watu walikuwa wamezoea vya bure
wanapiga 'disco' tu wanapewa hela nyingi hazipo pesa za namna hiyo, hivi sasa
watu wanataka ufanye kazi uzalishe mali ili upate fedha za kweli na asiyefanya
kazi asile na usipokula maana yake ufe" alisisitiza Rais
Magufuli
Mbali na hilo Rais
Magufuli amesema uchumi wa Tanzania unakuwa kwa kasi kubwa na kudai kwa Afrika
katika nchi tano ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi kubwa Tanzania pia ipo
imeshika nafasi ya pili nyuma ya Ethiopia.
"Ikiwa uchumi wetu unakuwa kwa asilimia 7.2%
wapo watu watakuja na kulalamika hela zimepotea, hao walikuwa wamezoea vya
bure, na hao ndiyo mnawaona wanapiga kelele" alisema Magufuli
No comments:
Post a Comment