Mkuu wa
Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza kwenye
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe.
Madiwani wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa
Geita wakati alipokuwa akitoa maelekezo na ushauri.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Nicas Mayala akisisitiza kufanyia kazi
ushauri ambao wamepatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Mkurugenzi
wa NGM GOLD MINE Emmanuel Gungu Siganga akipokea cheti cha Pongezi Kutoka kwa
mmwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kwa kuwa mdau mkubwa wa
kuchangia maendeleo kwenye sekta mbali mbali Wilayani Humo.
Baadhi ya wakuu wa Idara wakiwa kwenye
Mkutano wa Baraza la Madiwani Wilayani Bukombe.
Rai hiyo ameitoa Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel
Kyunga kwenye Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
.
Ambapo amesema kuwa Halmashauri Nyingi ikiwemo ya Bukombe ina maeneo
mengi ambayo yanauwezo wa kuwavutia wawekezaji tatizo kubwa ni kutokutangaza
fursa hizo.
“Kwasababu mwenye macho aambiwi tazama sisi wote jamani tunaona kwenye
Vyombo vya habari namna halmashauri mbali mbali zinavyochachalika kutangaza
Fursa zao halmashauri unakuta imejiwekea utaratibu inatangaza yenyewe fursa
inaita wawekezaji mbali mbali jamani ninachotaka kusema tuchachalike fursa
tunazo na tuzitangaze tuone ni wapi ambapo tunaweza kupata
wawekezaji”Alisisitiza Kyunga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukombe,Nicas Mayala amemwakikishia Mkuu wa
mkoa kuanza kufanyia kazi maelekezo na ushauri ambao ameutoa kwenye Halmashauri
Hiyo huku akiwataka wawekezaji kuja kuwekeza Bukombe kutoka na na kuwepo kwa
mifugo mingi ya Ng’ombe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Hiyo,Dionis Myinga amehaidi kufuatilia
na kutafuta wawekezaji ambao wataweza kuwekeza kwenye Wilaya Hiyo na
kwamba bado kunafursa nyingi za uwekezaji .
Hatua hiyo imekuja ni kutokana na halmashauri hiyo ,Mkoani
Hapa Kuwa na Idadi Kubwa ya Mifugo ikiwemo Ng’ombe.
No comments:
Post a Comment