Kiongozi wa
mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa,Amour Hamad Amour,amewataka Watanzania kujenga
desturi ya kupenda kununua Bidhaa ambazo zinatengenezwa na
kuzalishwa hapa Nchini kwaajili ya kuendelea kuwanyanyua
wajasiriamali wadogo pamoja na kuinua kipato cha Nchi.hapa ni wakati
alipokuwa akionesha kitenge ambacho kimetengenezwa nchini.
Mradi wa
usambazaji wa maji ambao upo kijiji cha Kiliman
Kiongozi wa
mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa,Amour Hamad Amour,akiweka jiwe la Msingi kwenye
mradi wa maji
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa Amour
Hamad Amour amewataka Watanzania kujenga desturi ya kupenda kununua
Bidhaa ambazo zinatengenezwa na kuzalishwa hapa Nchini
kwaajili ya kuendelea kuwanyanyua wajasiriamali wadogo pamoja na
kuinua kipato cha Nchi
Rai hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizindua
klabu ya mapambano dhidi ya ukimwi kwenye shule ya Sekondari ya Zhakia Meghji
iliyopo Wilayani Chato Mkoani Geita,amesema kuwa Mikakati ya serikali ya
kuhakikisha kwamba wanakuza uchumi wa Taifa haitawezekana endapo kama
watanzania awatajari bidhaa ambazo zinatoka nchini Hapa.Aidha Amour ameendelea kusema kuwa katika kuhakikisha nchi inakuwa ni ya maendeleo ni lazima kuwepo kwa mikakati thabiti ya kupambana na mambo ambayo yamekuwa yakirudisha Nyuma maendeleo likiwemo swala la uvivu,maradhi na vitendo ambavyo vinakiuka misingi ya Nchi.
Sanjali na hayo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa ,ameweza
kutembelea na kuweka jiwe la Msingi kwenye mradi wa usambazaji maji ambao upo
kwenye Kijiji cha mlimani.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo ,kaimu mhandisi wa maji
kwenye Halmashauri hiyo Mali Msango ,amesema kuwa mradi huo umeanzishwa kwa
lengo la kuwapatia maji safi na salama na zaidi ya wananchi elfu ishirini na
tano wananufaika na mradi huo.
Wakazi wa Chato,Maria Malare na Richard Bagolele,wamesema kuwa kuwepo kwa
mradi huo na kuongezwa kwa Matanki imeleta msaada Mkubwa sana kwani walikuwa
wakipata shida hapo awali Tofauti na sasa.
Miradi ambayo imepitiwa ni 12 na ambayo imezinduliwa ni saba,minne
imetembelewa na mmoja utawekewa jiwe la msingi ambapo miradi yote ina thamani
ya shilingi ,2,042,896,037.50 kati ya fedha hizo wahisani
wamechangia shilingi,1,255.611.875,serikali kuu 691.808.162.50 halmashauri
91.020.00 na wananchi shilingi 4.456,000.
No comments:
Post a Comment