Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani)wakati wa hafla ya kumkabidhi Bendera ya Taifa Bi. Julietha Kabete (kushoto) Mrembo atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika 2016 nchini Nigeria.
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga ( katikati)
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam (hawapo
pichani) kuhusu mchakato wa kumpata mshiriki wa mashindano hayo kutoka kwa
washiriki wa Miss Tanzania 2016 wakati wa hafla ya kumkabidhi Bendera ya Taifa
Bi. Julietha Kabete(kushoto) Mrembo atakayeiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya Miss Afrika 2016 nchini Nigeria kulia ni Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ameahidi kuendelea
kufanya mageuzi makubwa katika mashindano ya urembo hapa nchini ili kuondoa
dosari zinazojitokeza katika mashindano hayo.
Mhe. Nape ametoa ahadi
hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati akimkabidhi Bendera Mshiriki wa Tanzania
katika mashindano ya urembo Bara la Afrika kwa mwaka 2016 yatakayofanyika
Novemba 28 mwaka huu nchini Nigeria.
Mhe Nnauye ameongeza
kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa mashindano kama haya yanakuwa na
tija kwa Taifa hasa katika kuleta ajira kwa vijana pamoja na kuitangaza nchi
kimataifa kupitia urembo.
“Serikali nia
yake ni kuhakikisha kuwa jambo hili linakuwa bora, linaminiwa na kuheshimika
hivyo watanzania wote watajivunia uwepo wa mashindano ya urembo
nchini” alisistiza Mhe Nnauye.
Aidha Mwakilishi wa
Millen Magese group Ltd Bw. Matukio Aranyande Chuma amesema kuwa shindano hili
litailetea sifa Tanzania na ni kwa mara ya kwanza kufanyika hivyo wataitumia
fursa hiyo kuitangaza nchi kimataifa kupitia urembo.
“ kwa niaba ya Millen
Magese group Ltd tunatoa shukrani zetu kwa Serikali na Kamati ya Miss Tanzania
kwa kutuunga mkono katika jambo hili na tunaahidi kufanya vizuri katika
mashindano haya”Alisema Bw. Chuma.
Kwa upande wake
Mshiriki kutoka Tanzania anayekwenda kushiriki mashindano hayo Bi. Julietha
Kabete ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuunga mkono mashindano mbalimbali ya
urembo Tanzania inaposhiriki.
“Naahidi kuitangaza
nchi yangu vizuri katika mashindano haya na naomba watanzania waniombee na
wanipigie kura ili niweze kushinda na kuitangaza Tanzania kimataifa katika
urembo” Alisema Bi Julietha.
Mashindano ya Miss
Afrika yameanzishwa mwaka 2016 na Prof. Bena Yage ambaye ni Gavana wa Jimbo la
Cross River nchini Nigeria kwa lengo kupata mabalozi wa nchi za Afrika
watakaosaidia kutangaza na kuelimsha waafrika kuhusu uchumi unaozingatia
utunzaji wa mazingira.
No comments:
Post a Comment