Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi Mhe. Hamadi Massauni akijibu
hoja mbalimbali za wabunge katika mkutano watano wa Bunge la 11 linaloebdelea
Mjini Dodoma Novemba 7, 2016.
Jumla ya askari 152 wamefukuzwa
kazi mwaka huu na Jeshi la Polisi kwa sababu ya kukiuka Sheria, Taratibu na
Kanuni ya Jeshi hilo kama zilivyoainishwa katika Kanuni za Kudumu za Polisi
(PGO) namba 103.
Idadi ya askari hao waliofukuzwa
kazi imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.
Maryam Msabaha aliyehitaji kufahamu juu ya idadi ya askari waliochukuliwa hatua
kwa sababu ya utovu wa nidhamu.
Mhandisi Masauni amesema kuwa kazi
ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama ni kulinda raia, mali zao pamoja na mipaka ya
nchi lakini kuna baadhi ya askari hao wanakwenda kinyume na Sheria kwa kuwapiga
wananchi na kuwasababishia ulemavu pamoja na vifo hivyo Jeshi hilo limewachukulia
hatua za kinidhamu.
“Jeshi la Polisi hufanya kazi kwa
mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo lakini kuna baadhi ya askari
wamekuwa wakikiuka maadili na mwenendo mwema wa Jeshi letu hivyo kuanzia
Januari 2015 hadi Juni 2016 tuliwachukulia hatua za kinidhamu askari 200”,
alisema Mhandisi Masauni.
Naibu Waziri huyo amefafanua kuwa
baada ya askari hao kuchukuliwa hatua za kinidhamu, walifanyiwa uchunguzi wa
kina na jumla ya askari 152 kati ya 200 walikutwa na hatia hivyo hatua
iliyofata ni kuwafukuza kazi.
Akizungumzia kuhusu mpango wa
Serikali juu ya kujenga nyumba za askari Polisi, Mhandisi Masauni amesema kuwa
wanatambua tatizo la makazi ya Askari Polisi katika maeneo mbalimbali nchini
hususani kwenye mikoa mipya hivyo Serikali ina nia ya kutatua tatizo hilo kwa
kuanza ujenzi wa nyumba kwa ajili ya askari hao.
“Serikali imedhamiria kupunguza
tatizo la upu ngufu wa makazi ya askari polisi kwa kujenga nyumba kwa awamu
kupitia mpango wa ujenzi wa nyumba 4,136 nchi nzima ambao utaanza kutekelezwa
baada ya taratibu za mkopo wa kuwezesha ujenzi huu kukamilika”, aliongeza
Mhandisi Masauni.
No comments:
Post a Comment