Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na washiriki wa
mashindano ya SHIMMUTA wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo Novemba 24, 2016
yanayofanyika Jijini Tanga
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
akicheza muziki aina ya kwaito pamoja na wachezaji na viongozi wa timu shiriki
wakati wa sherehe za uzinduzi wa mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini
Tanga
Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amekemea vikali baadhi ya
tabia ya viongozi wa timu zinazoshiriki michezo mbalimbali kutumia wachezaji
wasiostahili kutumika katika mashindano husika.
Ameyasema hayo wakati
akizindua mashindano ya michezo mbalimbali yanayoandaliwa na Shirikisho la
Michezo ya mashirika ya Umma na Binafsi (SHIMMUTA) yanayoendelea Jijini Tanga
ambayo yameshirikisha timu mbalimbali kutoka mashirika ya Umma na Binafsi
Tanzania.
Mhe. Nnauye amewataka
viongozi wa SHIMMUTA kufanya uhakiki upya wa wachezaji wa timu shiriki ili
kuondoa lawama zinazoweza kutokea na kupata mshindi anayestahili kwa kufata
Sheria na taratibu zote za mashindano.
“Nawaomba viongozi
muangalie na kupitia upya wachezaji wa timu shiriki ili kusiwe na zengwe lolote
katika mashindano haya na mshindi katika kila mchezo apatikane kihalali”
alisisitiza Mhe. Nnauye.
Aidha ametoa wito kwa mashirika
kutenga muda na fedha ili kuwezesha timu zao kushiriki katika michezo ikiwa ni
moja ya kujenga mshikamano na amani kwa watanzania na pia kujenga afya ya mwili
na akili.
Mashindano ya SHIMMUTA
yameshirikisha mashirika ya Umma na Binafsi katika michezo 12 ikiwemo Mpira wa
Miguu(Football), Mpira wa Pete(Netball),kuvuta kamba, Riadha, Mchezo wa
vishale(Darts),Mchezo wa Pooltable, mchezo wa bao, Karata,kukimbia na magunia.
No comments:
Post a Comment