MtendajiMkuuwaWakalawaUfundinaUmeme TEMESA Dkt. MussaMgwatu ( kushoto)
akizungumza na Meneja wa TEMESA Kigoma Mhandisi Hassan Karonda (kulia)
alipotembelea kituoni hapo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu(
mwenyeshaji la rangi yabluu) akijadili jambo na mafundi wa karakana ya TEMESA
Kigoma alipotembelea kituoni hapo kujionea utendaji kazi.
Mtendaji Mkuu wa
TEMESA Dkt. MussaMgwatu (aliyeketi) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalam
James Frank jinsi mfumo wa kielektroniki wa kukatishia tiketi katika kivuko cha
Ilagala Mkoani Kigoma unavyofanya kazi.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (wa
pili kulia) akiongozana na Meneja wa TEMESA Kigoma Mhandisi Hassan Karonda
(kulia) baada ya kukagua kivuko cha MV. Malagarasi kinachotoa huduma ya usafiri
katika Mto Malagarasi kati ya Ilagala na Kajeje mkoani Kigoma.
Shirika la umeme
Tanzania TANESCO linadaiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Kigoma kiasi
cha shilingi milioni 41 ikiwa ni malimbikizo ya madeni kutokana na matengenezo
ya magari mbalimbali yaliyofanywa na shirika hilo mkoani humo.
Hayo yameelezwa na
Meneja wa TEMESA Mkoa wa Kigoma Mhandisi Hassan Karonda alipokuwa akitoa
taarifa ya utendaji kazi kwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu
alipotembelea kituoni hapo.
Meneja huyo ameeleza
kuwa kwa sasa TEMESA Kigoma ipo katika operesheni ya kukusanya madeni kutoka
kwa Taasisi na makampuni wanayoyadai.
“Mtendaji Mkuu
tunazidai Taasisi mablimbali kiwemo Shirika la Umeme Tanzania TANESCO shilling
million 41 mpaka sasa” alisema Mhandisi Karonda.
Hata hivyo Dkt. Mgwatu
alimtaka Mhandisi Karonda kuhakikisha kuwa anakusanya madeni yote
anayodai mkoani humo haraka iwezekanavyo.
“ Fuatilia ofisi
kwa ofisi kukusanya madeni ili kukiwezesha kituo hiki kufanya kazi zake kwa
ufanisi mkubwa” alisisitiza Dkt. Mgwatu.
Akiwa katika ziara ya
kikazi mkoani humo Dkt. Mgwatu pia alipata fursa ya kutembelea kivuko cha
MV. Malagarasi na kuona utendaji kazi wake.
Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt Mussa Mgwatu yupo katika ziara ya
kutembelea vituo vya TEMESA nchi nzima kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo.
No comments:
Post a Comment