Sunday 27 May 2018

WANAFUNZI WA MADARASA YA MEMKWA, AWALI NA LA KWANZA KUNUFAIKA NA PROGRAM YA KKK GEITA



Wanafunzi wa madarasa ya  awali la kwanza na walioko nje ya mfumo wa elimu MEMKWA katika halmashauri ya mji wa Geita Mkoani humo wameendelea kunufaika na mpango wa KKK tatu ikiwa ni mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa Kusoma, Kuandika na kuhesabu.


Hatua hiyo inatokana na serikali kutambua kuwa elimu ni msingi kwa kila mtoto ambaye kwa namna moja au nyingine alikosa nafasi ya kujiunga wakati akiwa katika umri ambao unatakiwa hivyo kupitia  Darasa la MEMKWA litamwezesha kufikia malengo yake.

Kwa kuzingatia kuwa Elimu ni silaha muhimu kumkomboa  mtoto kifikra, Serikali ilianzisha programu ya  Mpango wa Elimu ya Msingi Kwa Watoto Walioikosa (MEMKWA) ili kuwawezesha watoto kupata elimu  nje ya mfumo rasmi.

Marko John ni moja kati ya wanafunzi wa shule ya msingi mseto amesema sababu ya yeye kuchelewa shule ni kutokana na wazazi wake kutafarukiana na kujikuta akiishi kwa bibi yake kijijini ambaye na yeye akuwa na uwezo wa kumtunza.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi,Grace  Mutabuzi ameelezea changamoto ambazo zimekuwa zikiwakumba watoto wanaosoma madarasa ya MEMKWA ni pamojana na wengi wao kuwa na majukumu ya kifamilia kwa maana ya uangalizi wa familia zao.

Afisa Elimu msingi Halmashauri ya Mji wa Geita Yese Kanyuma amesema kumekuwepo na mafanikio makubwa kwa baadhi ya wanafunzi wa darasa la MEMKWA ni kutokana na ushirikiano baina ya jamii ambayo inatamani kumuona mtoto anaelimika.

Programu ya MEMKWA ilianzishwa kwa majaribio kati ya mwaka 1999 hadi 2002 katika wilaya za Musoma Vijijini, Kisarawe, Ngara, Masasi na Songea Vijijini.  Programu hiyo ilipoonyesha mafanikio, mwaka 2003 serikali ilianzisha madarasa ya MEMKWA katika shule za msingi nchi nzima.

No comments:

Post a Comment