Sunday 28 February 2016

LEO KATIKA HISTORIA, TAREHE 28 FEBRUARY.


Bendera ya Misri.

Miaka 93 iliyopita katika siku kama ya leo , nchi kongwe ya Misri ilipata uhuru. Misri ilikombolewa na Waislamu miaka 20 baada ya kudhihiri dini tukufu ya Kiislamu. Mwaka 969 nchi hiyo ilidhibitiwa na kutawaliwa na silsila ya Fatimiyya hadi mwaka 1172 ambapo utawala huo ulipinduliwa na Waayyubi.

 Baada ya hapo Misri ilidhibitiwa na tawala tofauti. Waingereza walianza kuwa na ushawishi huko Misri katika miongo ya mwishoni mwa karne ya 19. Hata hivyo wananchi wa Misri walikabiliana na ukoloni wa Uingereza na mwanzoni mwa Vita vya Kwanza vya Dunia hapo mwaka 1914 Uingereza iliitangaza Misri kuwa chini ya himaya yake.


Wananchi wa Misri walidumisha mapambano ya uhuru baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia na kuilazimisha Uingereza kuutambua rasmi uhuru wa nchi hiyo hapo mwaka 1922. 

                                                              ***********

                               Raisi mstaafu wa 41 wa Marekani, Gorge Herbert Walker Bush.

Siku kama ya leo miaka 24 iliyopita, George Bush “baba” alitangaza usitishaji vita vya Ghuba ya Uajemi vilivyodumu kwa muda wa siku 40.

 Mgogoro huo ulianza mwezi Agosti 1990 baada ya majeshi ya Iraq kushambulia ghafla sehemu ya ardhi ya Kuwait na kuikalia kwa mabavu. Ndege za kijeshi za Marekani, Uingereza na Ufaransa zilianza kuyashambulia majeshi ya Iraq baada ya utawala wa Saddam Hussein kukataa amri ya kuyaondoa majeshi yake nchini Kuwait.







No comments:

Post a Comment