Sunday 18 September 2016

PICHA MBALIMBALI ZA MAADHIMISHO YA MIAKA MIWILI YA STORMFM RADIO KATIKA UWANJA WA DESIRE PARK



Baadhi ya Wafanyakazi na Watangazaji wa Stormfm wakibadilishana mawazo siku ya Jana katika Ukumbi wa Desire Park


Wakiwa katika picha ya pamoja Baadhi ya Wafanyakazi na Watangazaji wa Stormfm



Watangazaji wa Kipindi cha Storm Asubuhi katika picha ya pamoja, kulia ni Helena Maduhu, kati ni Joel E.Maduka na kushoto ni Paul Williams.


Watangazaji wa Kipindi cha Kijiweni wakiwa na Dj, Kulia ni Orest Ngowi,kati ni Ester Mabula na Kushoto Ni Deejay Kg


Tukio la kukata keki lilianza lakini picha kwanza kabla ya kukata


Muda wa Maakuli na Pichani ni Mkurugenzi wa Vipindi(PM) Chris Lugoe akipata chake


Kijiweni Masters Orest Ngowi na Ester Mabula 

Kwanza Shukrani za Dhati kwa  Mwenyezi Mungu kwa upendeleo wake kwetu sote kwa kutubariki na kutupatia pumzi ambayo tunatumia bila gharama yoyote ,Tunachukua nafasi hii kukushukuru sana wewe msikilizaji pamoja na mtembeleaji wa mitandao yetu ya Kijamii ikiwa Instagram,Facebook,Twitter,Tovuti pamoja na Blog yetu ambae umeendelea kutufatilia kwa vipindi mbali mbali vinavyorushwa na kituo chako bora cha matangazo kanda ya ziwa Ukuwa ndani na nje ya mkoa wa Geita.

Storm fm ni Kituo cha radio kilichopo Mkoani Geita,ambacho kinasikika kanda ya ziwa na kwa njia ya mitandao kama Tovuti yetu ambayo ni Stormfm.co.tz pamoja na Tunein, Ni kituo cha Biashara kilichoanzishwa tarehe 18 September 2014 na  leo hii kinatimiza miaka Miwili Tangu kuanza Shughuli za Utangazaji

Kimeendelea kuwa Mkombozi Mkubwa kwa Kuhabarisha,Kuelimisha,Kuasa na Kuburudisha kupitia vipindi mbali mbali ambavyo vimekuwa vikifanyika kituoni  hapo.

Ahadi ambayo timu nzima ya Stormfm inatoa kwako ni Kutanua wigo mkubwa wa matangazo ili kufikia idadi kubwa ya Watanzania pamoja na kutoa habari na taarifa zenye Uhakiki na Sahihi kwako.

Miaka Miwili Kwenye Kasi tunasema Spidi Bado Ni Ileile.


Asante Kwa Ushirikiano Wako.


No comments:

Post a Comment