Sunday 27 May 2018

TFDA YATOA NENO KWA WANANCHI WOTE NCHINI


Mamlaka ya chakula na dawa nchini imewashauri wananchi kuendelea kuepuka kubeba na kuhifadhi chakula cha moto kwenye mifuko ya plastiki kwa madai kuwa mifuko hiyo ikipata joto hutoa kemikali ambayo huingia kwenye chakula na kuleta madhara ya kiafya.

Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi wa dawa na vifaa nyongeza wa taasisi hiyo Bw. Ansikari Fimbo katika kikao kazi cha wahariri na waandishi wa habari wa mikoa ya Geita na Kagera kilicho fanyika kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa kagera,  kilicho lenga kuwataka wanahabari kuieleza jamii kuhusu kazi zinazo fanywa na mamlaka hiyo.

Amewashauri baadhi ya wananchi kuacha mazoea ya  kubeba na kuhifadhi chakula chenye joto kwenye mifuko ya plasitiki kwa kuwa mifuko hiyo ikichemka hutoa baadhi ya kemikali.

Aidha kwa upande wake meneja mawasiliano na uhusiano wa umma wa mamlaka ya chakula na dawa nchini Bi Gaudencia Simwanza ameiomba jamii kuendelea kushirikiana kwa kutoa taarifa pale wanapo baini uwepo wa bidhaa feki za chakula dawa na vipodozi kwenye maeneo yao.


No comments:

Post a Comment