Thursday 31 May 2018

WATU ZAIDI YA MILIONI 7 WANAFARIKI KWA MATUMIZI YA SIGARA


Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema uvutaji wa sigara unabaki kuwa chanzo kikuu cha vifo ambavyo vingeepukika licha ya kupungua kwa matumizi ya sigara duniani tangu kuanza kwa karne ya 21. 


Kwa mujibu wa WHO, zaidi ya watu Milioni 7 bado wanafariki kila mwaka kutokana na maradhi yanayosababishwa na uvutaji wa sigara. Hata hivyo uvutaji wa sigara duniani umepungua hadi asilimia 20 kati ya 2000-2016 kutoka asilimia 27.

No comments:

Post a Comment