Thursday 3 May 2018

SERIKALI MKOANI GEITA KUPUNGUZA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA DAWA NA VIFAA TIBA




Serikali mkoani Geita kupitia mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) unaotekelezwa katika Mikoa mitatu hapa nchini kwa kushirikiana na Serikali ya Uswis  imekusudia kuendelea kupunguza Changamoto za upatikanaji wa Dawa pamoja na Vifaa tiba kwenye Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati.
Akifungua mafunzo ya siku tatu wilayani Bukombe kwa Wakuu wa Idara za Afya kutoka  Halmashauri zote Mkoani hapa Katibu Tawala wa mkoa wa Geita Bw. Selestini Gesimba amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wa kuingia kwenye mfumo mpya wa matumizi ya fedha pamoja na ununuzi wa dawa na vifaa tiba.

Aidha kwa upande wake Mshauri wa Menejimenti ya dawa katika mradi huo Bi. Fiona Chilunda amesema mafunzo hayo yanajikita katika malengo makuu matatu ambayo ni NHIF iliyo boreshwa , JAZIA pamoja na Matumizi ya fedha kwenye Vituo vya Afya.

Kwa upande wa baadhi ya Washiriki wa Mafunzo hayo akiwemo Mganga mkuu wa wilaya ya Chato Dkt. Athanas Ngambakubi na Kaimu Mganga mkuu wa wilaya ya Bukombe  Dkt. Irine Mkerebe wamesema kupitia mafunzo hayo itasaidia kupunguza baadhi ya Changamoto katika Idara ya Afya mkoani hapa.

No comments:

Post a Comment