Thursday 24 May 2018

AJALI YASABABISHA KIFO CHA MTU MMOJA NA KUJERUHI WENGINE WATATU MKOANI GEITA







Mtu mmoja ambaye amejulikana kwa majina ya Maneno Eliasi mwenye umri wa miaka 18 amefariki dunia kutokana na ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Mkwema lenye namba za usajili T765 DCU aina ya TATA huku watu watatu wakijeruhiwa

Ajali hiyo imetokea kwenye Barabara ya soko la Nyankumbu Mjini Geita ambapo imeelezwa Dereva wa basi hilo alikuwa akijaribu kumkwepa mwanafunzi ambaye alikuwa akivuka hali ambayo ilisababisha kushindwa kumudu gari hilo kutokana na kukata kona kubwa iliyosababisha kuwapalamia waendesha baiskeli wawili walio kuwa upande wa kulia

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo amesema hadi sasa bado hawajabaini chanzo cha ajali hiyo na kwamba wanawashikilia wafanyakazi wa basi hilo kwa mahojiano zaidi huku wakimtafuta dereva Bw. Charles Mtaluma ambaye alitoroka baada tu ya kutokea kwa tukio hilo.



No comments:

Post a Comment