Friday 29 September 2017

TANZANIA YAKABIDHIWA MASHINE YA KUTOA DAWA YA USINGIZI WAKATI WA UPASUAJI


Pichani ni muonekano wa mashine ya kutolea dawa za usingizi, ambayo imetolewa msaada na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ) leo Jijini Dar es Salaam. Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 imetolewa na Kampuni ya Kas Medics Limited ikiwa ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam. 



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kupokea msaada wa mashine ya kutoa dawa za usingizi zilizotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ). Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 imetolewa na Kampuni ya Kas Medics Limited ikiwa ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Idara kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya na  Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ) Rose  Mlay.

 

Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ) Rose  Mlay akielezea jambo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mashine ya kutoa dawa za usingizi iliyotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ). Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 imetolewa na Kampuni ya Kas Medics Limited ikiwa ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Afya, Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kas Medics Limited Nishitha Kulshreshtha  mara baada ya kukabidhiwa kukabidhiwa msaada wa mashine ya kutoa dawa za usingizi iliyotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ) kufuatia udhamini wa kampuni hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Idara kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya.



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipata maelezo kuhusu namna mashine ya kutolea dawa za usingizi inavyofanya kazi wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa mashine hiyo iliyotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ) leo Jijini Dar es Salaam. Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 imetolewa na Kampuni ya Kas Medics Limited ikiwa ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam.



Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekabidhiwa mashine maalumu ya kutoa dawa za usingizi kwa mama wajawazito wenye uzazi pingamizi  wakati wa upasuaji  kwaajili ya kuokoa maisha yao.

Akizungumza katika makabidhiano hayo leo Jijini Dar es Salaam Waziri mwenye dhamana ya Afya Mh.Ummy Mwalimu alisema kuwa, hiyo ni hatua kubwa katika kupambana na vifo vya  wakina mama wajawazito pamoja na watoto wachanga.

Waziri Ummy alitoa pongezi kwa watu waliojitolea kupanda mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuunga mkono kampeni ya kuokoa maisha ya mama na mtoto wakiongozwa na Dkt.Ahmed Mohamed Makuwani, ambapo alisema kuwa waliopanda mlima Kilimanjaro wamewezesha kupatikana kwa msaada wa mashine hiyo, hivyo akawashukuru na kuomba wadau wengine kuiga mfano huo.

“Tunawashukuru Utepe Mweupe wa Uzazi Salama kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kushirikiana na serikali ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo kwa watoto wachanga, hatua hii inatufariji sana na naomba watanzania na wasio watanzania wenye mapenzi mema na afya ya mama na mtoto kuendelea kusaidia juhudi hizi ”, alisema Waziri Ummy.

Akieleza mafanikio katika sekta ya Afya waziri Ummy alisema kuwa kuna zaidi ya vituo vya afya 480 nchi nzima na kati ya hivyo vituo 109 vinavyumba vya upasuaji ambayo ni sawa na asilimia 20 huku akibainisha kuwa kufikia Juni, 2018 serikali  inatarajia kujenga vyumba vya upasuaji 170 vitakavyosaidia upasuaji wa mama wenye uzazi pingamizi na  idadi hiyo itaongezeka  na kufikia vituo 279.

Aidha Waziri Ummy alisema kuwa licha ya kujenga vyumba hivyo watahakikisha upatikanaji wa vifaa, ujenzi wa maabara kubwa, wodi za kinamama pamoja na nyumba moja ya mtumishi katika vituo vya afya vyenye vyumba vya upasuaji.

Kutokana na mpango mkakati  wa kupambana na vifo vya wajawazito na watoto wachanga Serikali inatarajia kufikia asilimia 50 mpaka asilimia 80 ifikapo mwaka 2020 ambayo ni kampeni ya Serikali ya Awamu ya Tano inayotarajia kuzinduliwa hivi karibuni ijulikanayo kama ‘Jiongeze Tukuvushe salama’ kampeni ambayo inalenga kuwasaidia wakina mama wajawazito popote walipo ili kuokoa maisha yao.

Naye  Mratibu wa Utepe Mweupe Dkt. Rose Mlay alisema kuwa mashine hiyo ni maalum katika kunusuru maisha ya mama na mtoto lakini pia inaweza kutumika kwa mtu yeyote mwenye matatizo ya kufanyiwa upasuaji.

Kwa upande wake katibu mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya alisema mashine hiyo iliyotolewa na shirika la the Guardian Health yenye themani ya Shilingi milioni 55 ina ubora na kiwango cha kutosha katika kutoa huduma kwa mgonjwa wakati wa upasuaji.

“Mashine hii ni ya kipekee kwa sababu ina uwezo wa kutengeneza oksijeni na haihitaji mitungi ya gesi kwa hiyo ni mashine nzuri kwa wagonjwa na akinamama wenye uzazi pingamizi”, alisema Dkt.Mpoki.


Dkt. Mpoki alisema kilichopo sasa ni kufundisha wataalam watakaohusika na matumizi ya mashine hiyo ili waweze kuitumia ipasavyo na kuahidi kuwa atahakikisha inatunzwa ili iweze kudumu kwa muda mrefu. 


No comments:

Post a Comment