Sunday 27 May 2018

RC GEITA MHANDISI GABRIEL AONGOZA UJENZI WA NYUMBA 100 ZA ASKARI










Mkuu wa Mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel aongoza kampeni ya uzinduzi wa ujenzi wa nyumba 100 za askari Mkoani Geita ambao umefanyika eneo la Magogo.

Akiwa katika eneo hilo Mhandishi Robert Gabriel amewapongeza wananchi na wadau mbalimbali kwa kuonyesha uzalendo wao wa kujitoa kwa kiwango kikubwa kuchangia shughuli hii ya ujenzi wa nyumba za askari polisi.

Ameongeza kuwa tukio hilo ni mwendelezo wa kuimarisha taasisi na vyombo vya ulinzi na usalama kwani askari wamekuwa wakiishi katika maeneo yasiyo rasmi na yenye changamoto mbalimbali.

Katika tukio hilo wadau wamejitokeza na kutoa michango ya aina tofauti ikiwemo kujitolea kujenga maboma.kampeni hii imeanza kwa lengo la kujenga nyumba 50 kwa awamu ya kwanza. 
Aidha, katika eneo la Magogo Mhe. Gabriel amempongeza kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Geita kwa kazi nzuri ya kulinda amani Mkoani na kupunguza matukio ya uharifu.


No comments:

Post a Comment