Monday 21 May 2018

ACHOMWA MOTO NA WANANCHI KWA WIZI WA SHILINGI ELFU ISHIRINI GEITA


Baadhi ya wananchi wa mtaa wa kambarage 14 Kata ya Buha hala Mjini Geita wakiwa wanashangaa mwili wa marehemu Erick maarufu kwa jina la Whait baada ya kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali.

Wananchi wakiwa wanashangaa tukio hilo.


Duka ambalo alivunja marehemu na kuchukua kiasi cha  Sh,elfu 20 mtaa wa 14 kambarage.


Kamanda wa Polisi Mkoani Geita,Mponjoli Mwabulambo akithibitisha kutokea kwa tukio hilo.


Kijana aliyefahamika kwa jina moja la Erick mkazi wa Mtaa wa 14 Kambarage Kata ya Buhalahala wilayani Geita ameuawa kisha mwili wake kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali akituhumiwa kuvunja Duka la Bw Michael Yusuf na kuiba Sh elfu ishirini(20,000) .


Hatua hiyo imefikiwa baada ya wananchi kumtuhumu kijana huyo kujihusisha na uhalifu wa mara kwa mara na kwamba kipindi cha nyuma amewahi kuhusika na ubakaji wa Mwanamke mwenye umri wa miaka sitini (60).



Baadhi ya wananchi waliofika eneo la tukio wamesema kijana huyo amekuwa na kawaida ya kufanya uhalifu kwenye maeneo mbalimbali kabla ya kuuawa.


Tunasikitika sana na tabia ya baadhi ya vijana kushindwa kufanya shughuli kwa njia ya harari na kujipatia kipato matokeo yake wamekuwa wakitumia njia za panya kutafuta mafanikio ya haraka jambo ambalo sio sahihi kabisa mimi nisema hatua ambayo wameichukua wananchi sio nzuri ni bora wangeacha nyombo vya usalama vitatue tatizo hili”    Alisema Bi,Jamila Hassani.


Baadhi ya wazee wa mtaa huo wamesema vijana wanaojihusisha na uhalifu wamekuwa wakihifadhiwa na mmoja wa wananchi wa eneo hilo .


“Hapa mtaani kuna mkubwa wao ambaye amekuwa akiwatunza vijana hawa ingawa tunamjua ila hatutaki kumsema tumemuhifadhi siku nyingine tutamtaja endapo akiendelea na tabia hizi sisi wazee zinatuchukiza sana” Alisema Mzee Safari Malando.


Mwenyekiti wa mtaa huo Bw,Mfaume Nkerebe amesema anamfahamu marehemu kutokana na vitendo vyake vya uharifu na kwamba tukio hilo sio la kwanza kwani alishawai kuiba kwenye stational na kumbaka bibi kizee wa miaka sitini.


Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Bw Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiwataka wananchi kutokujichukulia sheria mkononi.

No comments:

Post a Comment