Wednesday 23 May 2018

WANAWAKE WAJAWAZITO WANATAKIWA KUHUDHURIA KLINIKI MARA KWA MARA KUZUIA FISTULA




 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wakati akitoa tamko la ugonjwa wa Fistula katika Ofisi ndogo  za Wizara ya Afya  Jijini Dar es salaam.



Mkurugenzi wa Shirika la AMREF  Afrika Dkt. Floriance Temu akiongea na waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa  fistula Duniani mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto Dkt. Faustine Ndugulile katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es salaam.


Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kimataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA) Bi. Jacqueline Mahon akiongea na waandishi wa habari mbele ya Waandishi wa habari na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.


Wanawake wajawazito wanatakiwa kuhudhuria Kliniki mara kwa mara ili kuangalia maendeleo ya ujauzito wao na kupata vipimo na matibabu kama itagundulika kuna uwezekano wa kupata ugonjwa wa Fistula.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo yaJamii, Jinsia,Wazee naWatoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kutoa tamko la ugonjwa wa Fistula katika kuadhimisha siku ya ugonjwa huo duniani.

Asilimia 60 ya wanawake nchini ndiyo wanahudhuria Kliniki mara kwa mara hii ni dalili mbaya kwani kama mwanamke mjamzito anaweza kuwa na viashiria vya Fistula hatoweza kugundulika mapema na kupata matibabu na badala yake asilimia 40  tu ndo wanaohudhuria Kliniki” alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kutokomeza ugonjwa huo Serikali kupitia Wizara ya Afya imeandaa mkakati wa kupeleka wataalam kwenye kila mkoa kujua idadi ya wagonjwa wa fistula ili kuweza kutokomeza ugonjwa huo.

Vilevile Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeimarisha na kukarabati vituo vya Afya vipatavyo 288 katika vitengo vya kuhudumia wenye uzazi pingamizi kwani hiyo nayo ni sababu inayopelekea wanamke kupata fistula.

Hata hivyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa huduma  za Fistula zinapatikana Bure nchini hasa kwenye hospitali za CCBRT, Bugando na Celian hivyo mwanamke akijiona ana dalili za ugonjwa huo anatakiwa kuwahi katika kituo cha kutolea huduma za afya na kupata Ushauri.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linaloshughulikia mambo ya afya Dkt. Frolence Temu amesema kuwa katika kupambana na ugonjwa wa Fistula nchini wanajenga uwezo kwa watumishi wa Hospitali za Wilaya naMkoa.

Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia idadi ya Watu UNFPA  Bi. Jacqueline  Mahon amesema kuwa Shirika hilo limetoa mafunzo kwa watoa huduma  za afya wapatao elfu nne ili kupambana na ugonjwa huo.

Mbali na kujengea uwezo watumishi hao pamoja na ukarabati wa vituo vya afya ,watanzania wanatakiwa kuacha vitendo vya udhalilishaji kwa wagonjwa wa fistula na wenye ugonjwa huu wajitokeze mara moja kwa ajili ya kupata matibabu” Alisema Bi. Mahon.

Mbali na hayo Mkurugenzi Mkuu wa uendeshaji hospitali ya CCBRT amesema inashirikiana na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Fistula Hospitali yake inafanya matibabu kwa wagonjwa 1500 kila mwaka .

Ugonjwa wa Fistula huadhimishwa Mei 23 kila mwaka na maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kaulimbiu isemayo“BILA YA KUMUACHA MWANAMKE YEYOTE MWENYE TATIZO LA FISTULA NYUMA SHARTI TUDHAMIRIE KUTOKOMEZA FISTULA SASA”

No comments:

Post a Comment