Thursday 3 May 2018

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI GEITA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI




Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Geita, GPC kimetangaza kuondoa zuio la kushirikiana na Jeshi la Polisi lililowekwa tangu mwezi January mwaka huu
Mwenyekiti wa Chama hicho mkoani Geita Bw Daniel Limbe ametoa kauli hiyo muda mfupi uliopita wakati akifunga mkutano wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Uhuru kwa Vyombo vya Habari uliofanyika kimkoa kwenye Hoteli ya Safety Park mjini Geita

Mmoja wa waandishi wa Habari Bw Mutta Robert amesema kuondolewa kwa zuio hilo kutarahisisha utendaji kazi unaohitaji ukauli ya jeshi la polisi

Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yalianzishwa mwaka 1993 baada ya kutangazwa kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa

No comments:

Post a Comment