Sunday 27 May 2018

WAKULIMA WA MPUNGA WAIOMBA SERIKALI KUBORESHA SOKO LA ZAO HILO GEITA


Mkulima wa mpunga kutoka kijiji cha Nyawilimelwa Bw Lazaro Lujina akizungumza juu ya hataua ya wao kuendelea kuhuza mazao yao kwa bei ya hasara.


Baadhi ya magunia ya Mpunga yakiwa kwenye ghara la kuhifadhia mazao hayo.


Bw. Rashid Kibashala  akizungumza juu ya hatua ya kuendelea kununua kwa bei za chini na wao kuhuza bei ya Juu

Ngunia ambalo wakulima wamekuwa wakililalamikia kuwa limekuwa likiwasababishia hasara kutokana na ujazo wake ulivyo.



Wakulima wa Mpunga kijiji cha Nyawilimelwa Wilayani Geita Mkoani humo wameiomba Serikali kuwatengenezea Soko la pamoja ambalo litasaidia kuuza mazao yao kwa bei nzuri zaidi kuliko sasa hivi ambavyo wamekuwa wakiuza bei ya hasara kwa walanguzi wanaoingia kijijini Humo.


Wakizungumza mtandao huu Kijijini hapo baadhi ya wakulima wamesema kukosekana kwa soko nzuri la kuhuzia mazao yao imekuwa ni sababu ya wao kuhuza kwa bei  isiyo nzuri na pindi wanapotaka kupereka mjini wamekuwa wakikutana na changamoto ya ubovu wa Barabara.

“Tatizo ni kukosekana kwa soko ndio sababu ambayo imekuwa ikisababisha sisi wakulima kushindwa kukaa na mazao kwa muda mrefu ndani na unakuta na sisi tunashida nadhani serikali ingeona umuhimu ikatutengenezea soko ingependeza zaidi kama vile pamba tunaona inasoko lakini mpunga hauna soko kabisa” Alisema Julius Mandegere.

Kutokana na malalamiko ya wakulima kunyonywa na baadhi ya walanguzi mtandao imezungumza na Mlanguzi wa mazao hayo,Bw Rashid Kibashala  ambapo amesema mala nyingi wamekuwa wakifanya maelewano kabla ya biashara.

“Kila biashara inamaelewano hivyo sisi tunafanya maelewano na wakulima juu ya bidhaa ambayo tunanunua kwa lengo la kwenda kupata faida siunajua kaka na sisi tunasafirisha hivyo tunaitaji faida sisi hatuwanyonyi” Alisema Kibashala.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho,Bw Majuto Mariatabu amesema hili kuwasaidia wakulima kutokuuza mazao yao holela wamekuwa wakiwakamata wale ambao wameendelea kuwagalaliza wakulima hao.

Afisa Kilimo wa Mji wa Geita,Bw  Samweli Ng’wandu akielezea namna ambavyo wametoa elimu kwa wakulima juu ya umuhimu wa utunzaji wa chakula hususani katika kipindi hiki cha mavuno.

No comments:

Post a Comment