Asilimia 71 ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli
tangu alipoingia madarakani. Kiwango hiki kimeshuka kutoka asilimia 96 mwezi
Juni 2016. Viwango vya kukubalika kwa Rais vinatofautiana katika makundi
mbalimbali
·
Asilimia 68 wenye umri chini ya miaka 30 wanamkubali Rais
ikilinganishwa na asilimia 82 wenye umri zaidi ya miaka 50
·
Asilimia 75 ya wananchi wenye elimu ya msingi au chini yake
wanamkubali Rais ikilinganishwa na asilimia 63 ya wale wenye elimu ya sekondari
au zaidi
·
Asilimia 75 ya wananchi masikini wanamkubali Rais ikilinganishwa
na asilimia 66 ya wananchi matajiri
Viwango vya kukubalika kwa viongozi wengine navyo pia vimeshuka
katika kipindi hicho hicho.
·
Wabunge: Kukubalika kwa utendaji wa wabunge kumeshuka kutoka asilimia
79 (Juni 2016) hadi asilimia 58 (Aprili 2017).
·
Madiwani: Kukubalika kwa utendaji wa madiwani kumeshuka
kutoka asilimia 74 (Juni 2016) hadi asilimia 59 (Aprili 2017).
·
Wenyeviti wa vijiji/mitaa: Kukubalika kwa utendaji wa wenyeviti wa vijiji/mitaa
kumeshuka kutoka asilimia 78 (Juni 2016) hadi asilimia 66 (Aprili 2017).
Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika utafiti wake uitwao
Matarajio na matokeo; Vipaumbele, utendaji na siasa nchini Tanzania.
Utafiti huo unatokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi,
utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za
mikononi.
Matokeo hayo yanatokana na takwimu zilizokusanywa mwezi Aprili
mwaka 2017 kutoka kwa wahojiwa 1,805 kutoka maeneo mbalimbali Tanzania Bara (Zanzibar
haihusiki kwenye matokeo haya).
Kukubalika kwa vyama vya siasa kunatoa taswira mchanganyiko.
Kukubalika kwa CCM kumeendelea kuimarika, ikiwa ni kati ya asilimia 54 na
asilimia 65 kati ya mwaka 2012 na 2017, Baada ya kushuka mwaka 2013 na 2014
ambapo kiwango cha kukubalika kilifikia asilimia 54 kutoka asilimia 65 ya
2012.
Kukubalika kwa CCM kumeendelea kubaki katika kiwango hicho hicho
cha asilimia 62 tangu uchaguzi wa mwaka 2015 na asilimia 63 mwaka 2017.
Kukubalika kwa Chadema kumeshuka hadi asilimia 17 mwaka 2017 kutoka asilimia 32
mwaka 2013.
CCM inakubalika zaidi miongoni mwa wazee (asilimia 80),
ukilinganisha na asilimia 55 ya vijana. Wanawake (asilimia 68) wanaikubali CCM
kuliko wanaume (asilimia 58), maeneo ya vijijini (asilimia 66) kuliko maeneo ya
mijini (asilimia 57), na wananchi masikini (asilimia 69) kuliko matajiri
(asilimia 53). Wananchi wenye elimu ya sekondari, elimu ya ufundi au elimu ya
juu wanaikubali CCM kwa asilimia 46.
Kukubalika kwa Chadema kwa ujumla unafuata mtiririko tofauti: ni
mkubwa miongoni mwa vijana, wanaume, watu matajiri na wenye kiwango kikubwa cha
elimu.
Ndani ya kipindi cha miaka miwili tu, vipaumbele vya wananchi
vimebadilika sana. Mwaka 2015, asilimia 34 ya wananchi walitaja umasikini na
uchumi duni kama moja ya vipaumbele vyao vikubwa ikilinganishwa na asilimia 60
waliotaja masuala hayo mwaka 2017.
Mwaka 2015, ni asilimia 9 waliotaja upungufu wa chakula au njaa
kama kipaumbele chao ikilinganishwa na asilimia 57 mwaka 2017.
Katika kipindi hicho hicho, wasiwasi wa wananchi juu ya huduma
za umma na rushwa umepungua.
Asilimia ya wananchi wanaotaja masuala yafuatayo kuwa miongoni
mwa changamoto kuu tatu zinazoikabili nchi:
·
Afya: asilimia 40 mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 59 mwaka
2015.
·
Elimu: asilimia 22 mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 44 mwaka
2015.
·
Miundombinu: asilimia 21 mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 32
mwaka 2015.
·
Huduma ya maji: asilimia 19 mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia
46 mwaka 2015.
·
Rushwa: asilimia 10 mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 28 mwaka
2015.
No comments:
Post a Comment