Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akikata utepe kama ishara ya kufungua jengo
jipya la ofisi ya TRA, Wilaya ya Chato, Mkoani Geita katika ufunguzi
uliofanyika leo mjini Chato.
|
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akipiga makofi baada ya kuwa amekata
utepe ambao unaashiria kufunguliwa kwa Jengo la mamlaka ya mapato Wilayani
Chato.
|
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
Majaliwa akihutubia wananchi wa Chato wakati wa ufunguzi wa jengo la TRA
wilayani humo mkoani Geita leo.
|
Jengo la mamlaka ya mapato(TRA)Wilayani Chato.
Waziri Mkuu,akiwapongeza
na kutoa zawadi kwa kwaya ya Mwagazege ambao walikuwa wakiimba nyimbo ya
kuipongeza serikali ya awamu ya Tano kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya chama
cha mapinduzi(CCM)
|
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga wakipongeza kikundi cha Kwaya kwa wimbo mzuri. |
Mkuu wa Wilaya ya Chato,Shaaban Ntarambe
akitambulisha wageni ambao walikuwepo kwenye viwanja hivyo.
|
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akiagana na Mkuu wa
Mkoa wa Geita.
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa na Mkuu wa Wilaya ya
Chato.
Mbunge wa Chato ambaye pia ni Naibu waziri wa
Nishati na Madini,Dk Medadi Kalemani akizungumza na wananchi.
Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere akitoa maelezo ya mradi
wa ujenzi wa ofisi ya TRA katika uzinduzi wa ofisi hiyo uliofanyika
leo katika wilaya ya Chato, mkoa wa Geita
|
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa,amesema kuwa kila mwananchi wa Tanzania
anawajibika kulipa kodi kwaajili ya ujenzi wa Taifa na kwamba uchumi
utajengwa na watanzania kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa kwani
kufanya hivyo itawaza kusaidia upatikanaji mkubwa wa kodi.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa zinduzi wa Jengo la mamlaka ya mapato
nchini(TRA)Wilayani Chato Mkoani Geita, ambalo ujenzi wake umeghalimu kiasi cha
Sh ,Bilioni 1.4.
Waziri Mkuu amesisitiza kuwa Kila
mwananchi ambaye anastahili kulipa kodi la lazima alipe bila ya kushurutishwa
kwani ni jambo la kawaidia na kwamba nchi ambazo zimeendelea ni kutokana na
wananchi wake kujenga destuli ya ulipaji wa kodi
Pia ameendelea kueleza kuwa Kutokana na maelekezo ya Ilani,Katika Mwaka 2016/17
Kuanzia Mwezi Julai,2016 hadi kufikia mwezi Aprili ,2017 Serikali imefanikiwa
kukusanya Shilingi Trilion 20.7 Sawa na Asilimia 70.1 na kwa lengo la mwaka
walijiwekea malengo ya kukusanya Sh,Trilion 29.5,Kati ya makusanyo hayo mapato
ya ndani ya kodi yalikuwa ni Sh,Trilioni 11.6 Sawa na Asilimia 77.1 ya lengo la
kukusanya Sh,Trilion 15.1
Aidha Waziri Mkuu ametoa Wito kwa Kila mwananchi kuakikisha anadai na kupewa
Risiti ya manunuzi ya bidhaa alizonunua na kwamba TRA ihakikishe kila
mfanyabishara anakuwa na mashine za kielektroniki.
Kamishina wa mamlaka ya mapato TRA Charles Kichere amesema kuwa
Pamoja na kuboresha miundo mbinu ya majengo Mamlaka imeanzisha mifumo ya
ukusanyaji mapato kwa njia za kielekitroniki ambazo zitaunganishwa na
ofisi hiyo ili kutoa huduma kwa urahisi kama ilivyo kwenye ofisi zingine
kote nchini.
"Baadhi ya huduma zitakazotolewa hapa ni kama; Utoaji wa Namba ya
Utambulisho wa Mlipakodi (TIN), utoaji wa leseni za udereva, huduma
za usajili wa magari, ukusanyaji wa kodi za majengo, na kodi zinginezo ambazo
zinasimamiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa mujibu wa Sheria"Alisema
Kichere.
"Haya yote yanafanyika kwa lengo la kuhakikisha kodi na tozo mbalimbali
zilizopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinakusanywa
kikamilifu ili kufikia lengo la makusanyo yanayokusudiwa katika mwaka ujao wa
Fedha na kuendelea"Aliseongeza Kichere.
Jengo hilo ambalo limefunguliwa leo lilianza kujengwa mnamo
tarehe 13 Julai, 2016 na kumalizika tarehe 12 Juni, 2017 ambapo kazi ya ujenzi
ilihusisha ujenzi wa jengo la ghorofa moja kama ambalo lina nafasi ya
kutosha kutoa huduma zote za kodi pamoja na huduma za kibenki ili kuwapunguzia
adha walipakodi kwa kupata huduma zote mahala pamoja.
Kampuni ambayo imejenga jengo hilo ni Wakala wa
Majengo Tanzania (TBA)na mjenzi ni kampuni ya Mayanga Constructions
ambapo katika ujenzi huu zimetumika kiasi cha Takriban Shilingi Bilioni 1.4.
No comments:
Post a Comment