Wachimbaji
wadogo wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Geita wakati alipokuwa akitoa maagizo.
Mkuu wa
Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akizungumza na Baadhi ya wachimbaji wadogo
kwenye mgodi wa Bakrif uliopo kwenye Kata ya Lwamgasa
Zaidi ya wachimbaji mia moja (100) wa kata ya Lwamgasa Wilayani Geita
wamevamia kwenye maeneo ya Mgodi wa Bakriff na kuanza shughuli za uchimbaji kwa
madai kuwa mwekezaji amemaliza muda wake ana hataki kuwapatia fidia ya maeneo
yao.
Akizungumzia juu ya tatizo ambalo limepelekea wachimbaji kuvamia
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Kwenye kata Hiyo Edward
Kiswaga ,amesema kuwa kuna watu ambao walitathiminiwa na walitakiwa kulipwa na
kwamba takribani miaka minne wamekuwa wakizungushwa juu ya kupatiwa fidia zao.
“Tuliwai kuja na Mheshimiwa Kalemani wakaahidi kwamba watajenga barabara
na kutoa huduma kwa wanajamii wa Lwamgasa lakini nimekuwa nikifuatilia
kwa Mheshimiwa Minda na nina wauliza kwa nini hamtekelezi ahadi zenu wamekuwa
wakisema Mkurugenzi yupo Canada huku kuna watu ambao tayari wameshatathiminiwa
wanatakiwa kulipwa fedha zao”Alisema Kiswaga
Kutokana na madai ya kutokulipwa fidia ya maeneo yao Meneja wa Mgodi wa
Bakriff, Peter Zichovu amesema kuwa walikuwa na mpango wa kuwalipa watu hao
lakini tatizo kubwa ambalo lilionekana ni watu kuongezeka na kwamba walikuwa
wana mpango wa kufanya tathimini na kuwalipa watu hao ambao wamekuwa na madai
ya fedha zao.
Kutokana na maelezo hayo Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ambaye
alikwenda kutatua shida hiyo kwa wananchi amesema kuwa tarehe 15
watakutana yeye na naibu Waziri kwenye eneo hilo na kwamba amewapa wachimbaji
hao siku tatu (3) kufanya shughuli za uchimbaji na baada ya hapo wayaachie
maeneo hayo hadi pale uwamuzi utakapofikia wa maeneo hayo.
Eneo la Bakriff lina leseni ya uchimbaji Mkubwa na kwamba leseni
hiyo inamilikiwa ubia kati ya shirika la madini la Taifa Stamico pamoja
na kampuni ya Tanzamu na kwamba leseni hiyo inadumu miaka kumi (10) na kwamba
imekwisha kumalizika lakini tayari wamekwisha fanya taratibu za
kubadilisha (kulinew) leseni hiyo ingawa bado haijawekewa saini na Waziri
mwenye dhamana.
No comments:
Post a Comment