Serikali kupitia
Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imesema imeandaa mtaala mpya ambao
umeandaliwa katika misingi ya elimu jumuishi ambao ulianza kutumika kuanzia
mwaka wa masomo 2014/2015 ili kumudu wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Hayo yamesemwa na Naibu
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Eng,Stella Manyanya wakati akijibu
swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Stella Ikupa Alex aliyetaka kujua Serikali
ina mpango gani wa kuhakikisha kila mwalimu anapatiwa mafunzo maalum
yatakayomwezesha kufundisha wanafunzi wenye ulemavu.
“Hadi sasa wahitimu wa
ngazi ya Stashahada ya Elimu maalum wapatao 158 wamehitimu Octoba 2016 na
wanachuo 248 wanaendelea na masomo katika chuo cha Ualimu Patandi”,Aliongeza
Mhe.Manyanya.
Aidha Waziri uyo
amesema kuwa kutokana na umuhimu wa walimu hawa Wizara yake katika mwaka wa
fedha 2016/17 iliendesha Mafunzo kwa walimu 519 walio kazini
wanaofundisha darasa la kwanza na la pili kuhusiana na mtaala
ulioboreshwa ili kumudu ufundishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Pamoja na hayo tarehe
20 mpaka 28 Juni,2017 walimu 712 walio kazini wanaofundisha wanafunzi wenye
ulemavu wa akili na wenye usonjo walipatiwa mafunzo katika vituo vya
Mwanza,Arusha,Mbeya na Morogoro ili kuwajengea uwezo wa kumudu ufundishaji wa
wanafunzi wenye ulemavu huo.
“Walimu 600
wanaofundisha darasa la tatu na nne watapatiwa mafunzo ya Mtaala ulioboreshwa
kuanzia tarehe 10 hadi 30 Julai,2017 lengo ni kuwafikia wengi zaidi”Alisisitiza
Mhe.Manyanya.
No comments:
Post a Comment