Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akitoa
maagizo kwa afisa Madini wa Mkoa wa Geita na Mkuu wa Polisi Wilayani humo
wakati wa Mkutano wa hadhara
Wananchi wa Kijiji cha Nyamtondo Kata ya
Kaseme Wilaya na Mkoa wa Geita Wamesikitishwa na kitendo cha mwekezaji wa
Mgodi wa Nyamahuna unao milikiwa na Albert Ruzika kushindwa
kutekeleza agizo la serikali la kujenga visima vitatu vya maji kijijini hapo.
Hatua Hiyo imekuja ni baada wa Mkuu wa Wilaya ya
Geita,Mwl Herman Kapufi kutoa agizo la kujenga visima hivyo mwaka jana
mwezi wa kumi na mbili na kwamba kufikia tarehe thelathini mwezi wa tano mwaka
huu wawe wamekamilisha ujenzi huo.
Akizungumza kwenye Mkutoni wa wananchi Diwani wa
Kata ya Kaseme Andrea Kalamla amesema kuwa hadi sasa kuna kisima kimoja tu
ambacho kimejengwa na chenyewe hakitoi maji hadi sasa hali ambayo imekuwa
ikisababisha wanakijiji kutembea umbali mrefu kufuata maji.
“Mkuu wa Wilaya ungekuwa umefika mapema
tungekupeleka kwenye kisima ambacho kimejengwa ambacho hakina ubora wowote
kabisa kwani tunavyozungumza hadi sasa kisima kimekauka na hakina maji kabisa
na mimi kila ninapofika hapa wanakijiji wamekuwa wakiniomba maji hali
ambayo imeendelea kuninyima amani”Alisema Kalamla.
Kwa upande wake meneja wa mgodi wa huo ,BW Simion
Lubamba ameelezea kuwa utekelezaji wa ahadi za mgodi kwa wananchi zilikwama
kutokana na uzalishaji kupungua hivyo amewaomba wananchi kumpa muda wa miezi
miwili atakuwa ametekeleza ahadi hiyo.
“Kweli
uhaba wa maji upo hapa kulingana na agizo lako ambalo uliliandika mwekezaji
nilimpa nakala kwamba anatakiwa kutekeleza ahadi hiyo mwezi wa tano tarehe
thelathini awe ametekeleza lakini alijibu kuwa hali ilikuwa ni mbaya hivyo
ameomba kwa wananchi wampe miezi miwili hatakuwa atahakikisha anatekeleza ahadi
hiyo”Alisema Lubamba.
Kutokana na maelezo hayo Mkuu wa Wilaya Mwl Herman Kapufi
akatoa maagizo kwa afisa madini juu kufungia mgodi huo hadi pale utakapo
tekeleza ahadi yake huku mkuu wa jeshi la polisi wilayani hapo akitakiwa
kuweka ulinzi wa kutosha .
Wanakijiji wa kijiji hicho wamepongeza kwa hatua
ambayo ameichukua Mkuu wa Wilaya huku wakidai ni bora wote wakakoswa.
Akizungumzia Sheria ya madini kuhusu wawekezaji
Afisa madini wa Mkoa wa Geita,Ally Said Ally amesema kuwa mwekezaji anapaswa
kutoa huduma za kijamii .
No comments:
Post a Comment